KISWAHILI FORM 3 END TERM EXAMS PLUS ANSWERS IN PDF

SHULE YA UPILI YA ULTIMATE ACHIEVERS

JINA………………………………………………………..NAMBARI………..

TAREHE………………………………SAHIHI………………………………

TATHMINI YA MWISHO WA MUHULA

KIDATO CHA TATU

MATUMIZI YA LUGHA NA FASIHI

MUDA: SAA 2  1/2

Maagizo

Jibu maswali yote katika sehemu ya ufahamu, isimujamii  na matumizi ya lugha.

Chagua maswali mawili katika sehemu ya fasihi.

 1. SWALI LA KWANZA – UFAHAMU

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

 

Inasemekana kwamba bila saa shughuli zote duniani zitakwama. Hii ndiyo maana mfumo wa saa umewekwa ili kuwawezesha walimwengu kutekeleza majukumu yao wakati ufaao. Saa ni kitambulisho cha ustaarabu. Kila mtu aliyetia kiguu shuleni hana budi kuvaa saa zilizotengenezwa kwa vito vya thamani kama dhahabu.Saa hupatikana kila mahali. Minara, majengo, magari, redio na hata simu za mkononi zina saa. Kwa nini basi watu wengi hasa waafrika hawazingatii saa? Kwani kuchelewa ni ada ya Mwafrika?

 

Hakuna dakika inayopita bila kisa cha  kuchelewa. Mikutano karibu yote huchelewa kuanza kwa sababu wahusika hawaji wakati ufaao. Ibada nazo hucheleweshwa kwa uzembe wa waumini.Na mazishi je?Taratibu hucheleweshwa vilevile.Ingawa hapa yaweza kufikiriwa kuwa pengine wampendao marehemu hawataki kuharakisha safari yake ya mwisho. Lakini hata arusi ambazo huwa na misururu ya mikutano ya maandalizi siku itimiapo shughuli huchelewa.Si ajabu sherehe kuendelea mpaka usiku ambapo ratiba ilionyesha ikome alasiri.

 

Uchunguzi unabainisha kuwa watu huchelewa kwa sababu mbalimbali. Sababu moja- wapo ni kutowajibika, yaani, wengi hawaoni umuhimu wa kuzingatia saa. Wengine hufanya hivi kwa kisingizio kuwa ni kawaida ya mwafrika kutozingatia muda. Huu ni upuuzi mtupu. Wazee wetu walizingatia muda ipasavyo tangu jadi ingawa hawakuwa na saa wala kalenda. Hii ndiyo sababu walipanda walipohitajika, wakavuna na hatimaye wakapika na kuandaa ipasavyo. Wahenga hawa walituachia methali nyingi kama funzo, kwa mfano “Chelewa chelewa utampata mwana si wako” na “Ngoja ngoja huumiza matumbo”

 

Watu wengine huchelewa kwa sababu ya kutojiandaa kwa yale yatakayojiri. Watu wasiopanga shughuli zao na kuzifanya kwa kushtukia aghalabu hushindwa kuhudhuria hata mahojiano ya kuajiriwa kazi kwa wakati ufaao. Hawa huwa neema kwa washindani wao.Kujitayarisha si jambo gumu. Anachopasa kujua mhusika ni saa ya miadi na hali ya usafiri. Hivi viwili vitamwezesha kujua muda wa safari na hivyo kukadiria wakati wa kuondoka. Ni wangapi wameona milolongo ya watu nje ya milango ya benki wakiwasihi mabawabu na pengine kuwahonga wawaruhusu kuingia?Hawa huwa si wageni.Ni wateja wanaojua ratiba ya kazi lakini hushindwa kupanga mwenendo wao barabara.

 

Mikutano, sherehe na shughuli nyingi huchelewa kuanza kwa saa nyingi kwa sababu eti mgeni mashuhuri amechelewa kufika. Muda wa kungoja huwa mrefu zaidi kutegemea ukubwa wa cheo cha mhusika. Watu hawa huchelewa makusudi kwa sababu pengine ya kiburi. Majivuno haya huwafanya wafurahi wanaposubiriwa na watu wadogo. Wakubwa hawa wanapofika, badala ya kuomba msamaha, hujigamba kuhusu majukumu yao mengi na makubwa.

 

Aidha kuna watu ambao hupenda kutekeleza mambo mengi kwa wakati mmoja. Tujuavyo ni kuwa mambo mawili yalimshinda fisi. Pia watu wanaposhika mengi, mahudhurio yao katika baadhi ya mambo hutatizwa na hivyo huchelewa. Isitoshe, kuna watu ambao hushindwa kuhudhuria shughuli kwa wakati ufaao kwa sababu ya uzembe. Watu wa aina hii hata wakipewa ratiba mapema, hujikokota na hivyo hupitwa na wakati.

 

Ingawa sababu tulizotaja hutokana na watu wenyewe, kuna zile zinazosababishwa na dharura nyingine. Hizi ni pamoja na misongamano ya magari, kuchelewa kwa vyombo vya usafiri na hata kuharibika kwa vyombo. Hii ndiyo maana inashauriwa kuwa mtu anapoamua kutekeleza jambo, atenge muda takribani wa dakika 30 kwa ajili ya dharura fulani. Kwa hivyo, hata anapopata tuseme pancha njiani, bado atafika kwa wakati ufaao.

 

Kuchelewa hakuudhi tu watu wanaocheleweshwa bali huwa na matokeo mengine mengi. Mara nyingi watu waliochelewa huharakisha mambo ili kufidia muda waliopoteza. Kama wana gari basi huzidisha kasi. Matokeo huweza kuwa ajali ambayo mara nyingine huleta vifo na ulemavu.

 

Ratiba ya mambo ichelewapo, watu waliofika mapema hupoteza muda kusubiri. Muda huu wangeutumia kwa harakati muhimu. Mfumo wa uchumi wa kisasa unahitaji mamilioni ya watu kukurubiana, kutagusana na kuendesha shughuli kwa ujima. Aidha watu hawana budi kubadilishana bidhaa na huduma. Mambo haya yanapotekelezwa basi gharama huwa kubwa. Tatizo hili hubainika sana katika afisi za umma.

 

Ni kawaida watu kufika kazini dakika nyingi baada ya wakati wa kufungua milango au kazi. Ajabu ni kuwa wafanyakazi wawa hawa huwa wa kuanza kufunga kazi kabla ya kipindi rasmi. Inakisiwa Kenya inapoteza shilingi bilioni 80 kila mwaka kupitia uzembe wa kutozingatia wakati.

 

Hebu tuchukue mfano wa vipindi vya masomo shuleni. Ikiwa mwanafunzi atachelewa kwa dakika tano kila  kipindi katika shule yenye utaratibu wa vipindi vinane kwa siku,hii ni sawa na kipindi kimoja. Ni kama kusema mwanafunzi atapoteza takribani miezi miwili ya mafunzo kila mwaka.

 

Mtu binafsi anapojipotezea wakati si neno. Tatizo ni kule kuwapotezea wengine kwa hivyo, kuna haja ya kulikabili tatizo hili ili kuliondoa. Jambo la kwanza ni kuweka sera ya kitaifa inayolenga kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuzingatia saa. Hali kadhalika kanuni iwekwe ya kuwafungia nje watu wanaochelewa kuhudhuria shughuli za mikutano au hafla. Wananchi nao wazinduliwe kuwa ni haki yao kufumkana muda wa shughuli unapowadia kabla mgeni wa heshima kufika. Nchi ya Ekwado (Ecuador) imefanikiwa kutekeleza haya. Kenya pia haina budi kuandama mwelekeo huo. Hii ndiyo njia mojawapo ya kufufua uchumi na kuhakikisha taifa linapiga hatua kimaendeleo.

 

Maswali.

 1. Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka.                                                                      (alama 1)

………………………………………………………………………………………………

 1. Wataje walio na mazoea ya kuchelewa kufika kwenye shughuli walizoalikwa.  (alama 2)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. Eleza sababu zinazofanya baadhi ya watu kuchelewa kufika kwenye shughuli walizoalikwa kwa wakati ufaao.                                                                            (alama 3)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. Kuchelewa kuna athari gani?                                                                                         (alama 3)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 

 

 

 1. Fafanua njia zilizopendekezwa za kuondoa tatizo hili la kuchelewa.              (alama 3)

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 

 1. Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumika katika taarifa.                (alama 3)
 • Ada

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 • Ujima

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 • Kufumkana

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1.  SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

 

 1. a) Bainisha mzizi, viambishi awali na tamati katika sentensi hii                     (alama3)

Asihukumiwe.

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. b) Andika kwa umoja                                                                                                (alama2)

Pulikeni wanetu, msicheze na dunia. Mnasikia?

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. c) Andika kwa msemo wa taarifa                                                           (alama3)

“Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni, kisha nitaondoka kwenda kwangu kesho,” Maria alimwambia Yusufu.

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. d) Akifisha sentensi hii                                                                                   (alama3)

Oh huu ndio mkutano aliotuitia mmoja wao aliropoka.

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. e) Toa mifano miwili ya;                                                                                            (alama4)
 2. i) Sauti ghuna ambazo ni vipasuo.

………………………………………………………………………………………………………

 1. ii) Sauti sighuna ambazo ni vikwamizo.

……………..……………………………………………………………………………………….

 1. f) Andika sentensi kwa kinyume.                                                                  (alama1)

Kijakazi aliangika vyombo vya tajiri wake.

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

 1. g) Mwajiri wao amekuja kuwalipa mshahara. Kanusha.                               (alama2)

…………………………………………………………………………………………………….

………………………………………………………………………………………………………

 1. h) Andika kisawe cha kielezi                                                                 (alama1)

……………………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………………….

 1. i) Ainisha nomino zilizopigiwa mistari katika sentensi ifuatayo.            (alama2)

Kikosi cha askari kiliwanasa wezi na kuwarejesha ng’ombe wa maziwa walioibiwa kutoka tarafa ya Kilibwoni.

……………………………………………………………………………………………………

……………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………….

 1. j) Bainisha kirai katika sentensi hii, na ueleze ni cha aina gani .                        (alama2)

Kitabu kizuri kimenunuliwa.

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 

 1. k) Iandike sentensi upya kulingana na maagizo

Mwanariadha mmoja tu ndiye aliyefuzu katika mbio hizo.(Tumia hakuna/ila)      (alama2)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. l) Tumia vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizoonyeshwa katika sentensi               (alama4)
 2. i) Safiri (tendewa) ……………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 3. ii) pa(tendeka)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. m) Eleza matumizi ya ‘ku’, ‘ji’ na ‘ki’ katika sentensi zifuatazo.                     (alama3)
 2. i) Kuliko na miti hakuna wajenzi ……………………………………………………………………………………………………..
 3. ii) Mimi ninajivunia nchi yangu ya Kenya

…………………………………………………………………………………………………….

iii)       Nikija nitakueleza ……………………………………………………………………………………………………..

 

 1. n) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale.                     (alama3)

Mama anapika vizuri.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 1. ISIMU JAMII
MWISHO

Kuna madai kwamba lugha ya kiswahili ni zao la lugha za kibantu. Kwa mfano mitano thibitisha madai haya.                                                                                                                        (alama 10)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 1. FASIHI                                                                                                           ALAMA 20

Jibu swali moja kutoka sehemu hii.

 1. HADITHI FUPI

 Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine Na Alifa Chokocho Na Dumu Kayanda

Mame Bakari

“..Yallahi, dunia gani ametuumbia?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
 2. Fafanua sifa tatu za mhusika katika dondoo hili Alama 6
 • Fafanua madhila anayoyapitia mwanamke katika jamii hii.            Alama 10
 1. Riwaya

Chozi La Heri                                                                                    Na Assumpta Matei

Wanawake katika riwaya ya Chozi la Heri ni mawakala wakuu wa ukiukaji wa haki za binadamu. Dhibitisha.                                                                                                            Alama 20

 1. Tamthilia

Kigogo                                                                                                na Pauline Kea

“…Lazima chatu mmoja atolewe kafara ili watu wajue kuwa usalama upo”

 1. Eleza muktadha wa maneno haya.            Alama 4
 2. Eleza sifa tatu za anayeambiwa maneno haya Alama 6
 • Eleza umuhimu wa anayeambiwa maneno haya Alama 4
 1. Taja na ueleze mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili.       Alama 2
 2. Eleza kinaya kinachojitokeza katika dondoo hili       Alama 4

ANSWERS

UFAHAMU

 1. Kuchelewa/kuchelewa ni ada ya mwafrika (alama 1)

                        Zingatia saa

 1. .Wahusika katika mikutano
 • Waumini
 • Maharusi
 • Waombolezaji (2 x 1 = 2)
 1. .Kutowajibika
 • Kutojiandaa kwa yale yatakayojiri
 • Kisingizio kwa kuchelewa ni ada ya Mwafrika
 • Kuchelewa kwa mgeni mashuhuri
 • Uzembe
 • Watu kupenda kutekeleza mambo mengi kwa wakati mmoja (3 x 1 = 3)
 1. . Huudhi watu
 • Ajali au hata vifi
 • Kupoteza muda kwa wanaomsubiri mtu fulani Afrika
 • Wanafunzi hupoteza muda mwingi wa mafunzo (3 x 1 = 3)
 1. . Kuweka sera ya kitaifa inayolenga kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuzingatia

saa

 • Kanuni iwekwe ya kuwafungia nje watu wanaochelewa kuhudhuria shughuli za mikutano au hafla.
 • Wananchi wazinduliwe kuwa ni haki yao kufumkana muda wa shughuli unapowadia kabla ya mgeni wa heshima kufika. (3 x 1 = 3)
 1. . Ada – desturi/tabia/mwenendo
 • Ujima – ushirika/umoja
 • Kufumkana – kutawanyika/kwenda zao (3 x 1 = 3)

 

 

MWONGOZO WA MATUMIZI YA LUGHA

(a)       Asi – viambishi awali

Hukum – mzizi

Iwe – tamati                                                                                        (1×3 = 3)

(b)       Pulika ü mwananguü, usichezeü na dunia. Unasikia?ü                  (½x4=2)

(c)       Maria alimwambia Yusuf kuwa/ ya kwamba yeye angewakaribisha wageni siku hiyo jioni kisha angeondoka kwenda kwake siku iliyofuata                                                     (3)

(d)       “üüAh!ü Huuü ndio mkutano aliotuita?ü” Mmojaü wao akaropoka.(½x6=3)

(e)       (i)        / b / d / g / – sauti ghuna – vipasuo

(ii)       / f / th / sh / h/ – sauti sighuna-vikwamizo                             (1X4=4)

(f)        Kijakazi aliangua vyombo vya tajiri wake                                        (alama 1)

(g)       Mwajiri wao hajaja kuwalipa mshahara                                            (alama 2)

(h)       Kisawe ni chagizo                                                                              (alama 1)

(i)        Kikosi cha askari – Jamii/ makundi

Ng’ombe – kawaida

Maziwa – wingi

Kilibwoni – pekee                                                                              (½ x4=2)

(j)        Kitabu kizuri – kirai nomino                                                             (alama 2)

(k)       Hakuna mwanariadha aliyefuzu mbio hizo ila mmoja                      (alama 2)

(l)        Kila sentensi

(i)        Safiriwa

(ii)       Peka                                                                                        (2×2=4)

(m)      ku        – mahali

Ji         – kirejeshi

Ki        – masharti                                                                               (1×1=3)

 

(n)       S                      KN+KT

KN                  N

N                  Mama

KT                   T+E

T                      Anapika

E                      Vizuri                                                              alama (6x½=  3)

 

 

            ISIMU JAMII

 • Kama yalivyo maneno ya lugha za kibantu, maneno yote ya Kiswahili yasiyo ya asili ya kigeni yanafuata utaratibu wa viambishi na mizizi.
 • Msamiati wa msingi wa lugha ya kiswahili ni ule ule unaojitokeza katika lugha za kibantu
 • Muundo wa maneno ya kiswahili kama yale ya lugha zakibantu ni wa silabi zilizounwa kwa irabu au konsonanti na irabu.
 • Maumbo ya maneno kwa Kiswahili na lugha za kibantu yana viambishi.

k.m mu-ndu.

m-tu

Ø Kuna mfanano wa kimsamiati katika lugha ya Kiswahili na lugha za Kibantu.

k.m kuhoa, korora, kooa.

Ulimi.lulimi

Ø Lugha ya Kiswahili mara nyingi huwa na muundo wa silabi wazi/huru. Mfumo huu vile

vile hudhihirika katika lugha nyingi za Kibantu.

Kikombe/shikombe.

Kitabu/shitapu.

Ø Nomino hupangwa katika ngeli kama tu ilivyo katika lugha nyingine za Kibantu.

A/WA Mtu anaenda.

Watu wanaenda.

M/A Mundu athi

Andu mathi.

Ø Upatanisho wa kisarufi ni sawa k.m Baba analima/Baba arima.

Ø Katika lugha za Kibantu kuna uwezekano wa kuunda maneno kutokana na aina nyingine

ya maneno. Mfano kuunda nomino kutokana na vitenzi.

Ø Mpangilio wa maneno katika tungo ni sawa.

Mtu anakuja leo/Mundu anecha juno

Ø Kuna mnyambuliko wa vitenzi katika lugha ya kiswahili jinsi tu ilivyo katika lugha

nyingine za Kibantu.

Lia – lilia/Rira – ririra.

Piga – pigwa/khupa- khupwa.                                                                        5×2=10

FASIHI                                                                                                           ALAMA 20

 1. HADITHI FUPI

 Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine Na Alifa Chokocho Na Dumu Kayanda

Mame Bakari

 1. Ni fikra/mawazo ya Sara

Yuko chumbani mwake

Baada ya kugundua ana mimba inayotokana na kubakwa na mtu asiyemfahamu

Anafikiria jinsi angelaaniwa na wazazi na mwalimu mkuu                   4×1=4

 1. Msamehevu-anamsamehe mbakaji

Mwoga-aliogopa kumwambia yeyote kuwa amebakwa akihofia kulaumiwa

Msiri-alipobakwa, hakumwambia yeyote

Msomi-aliendelea na masomo hata baada ya ujauzito

Mwenye utu/huruma-alikataa fikra za kuavya mimba.

Kadiria jibu la mwanafunzi           3×2=6

 • Kubakwa

Kuozwa kwa lazima

Unyanyapaa kwa sababu ya jinsia

Kupigwa kwa wale wameolewa

Kudhalilishwa kwa matusi

Kutwikwa mzigo wa malezi

Kubaguliwa katika uridhi/elimu

Kufanyizwa kazi za sulubu.                                                         5×2=10

 1. Chozi la Heri
 • Subira, Naomi na Mama Sauna wanasambaratisha asasi ya familia kwa kuwatoroka waume zao.
 • Mama Pete anamkataza Pete masomo ili amwoze kwa Mzee Fungo
 • Mama Pete anamwoza mwanawe Pete kwa lazima kwa mzee aliye na wake watatu
 • Mama Sauna anamdhulumu mwanawe Sauna kwa kumwonya dhidi ya kumwambia yeyote jinsi babake wa kambo amekuwa akimbaka.
 • Sauna anawaiba Dick na Mwaliko kwa lengo la kuwauza kwa Bi. Kangara.
 • Kangara anawatumia Watoto wadogo kwa biashara haramu -mapenzi na ulanguzi wa dawa za kulevya
 • Mama Kaizari anamdhulumu Subira kwa sababu ya tofauti za kiusuli-Bamwezi
 • Annette anahamia ughaibuni na kumwacha mumewe Kiriri akiteseka/kwa upweke
 • Mama Kipanga anakataa kumwambia Kipanga babake halisi ni nani.
 • Satua anamdhulumu Chandachema baada ya kuhamia nyumbani kwake-sukari na sabuni zinakwisha kwa haraka
 • Wanawake wanajifungua na kuwatupa Watoto jaani kama yule aliyeokolewa na Neema.
 • Pete anakunywa dawa ya kuulia panya ili afe.
 • Tuama anaunga mkono upashaji tohara wa wasichana
 • Tindi anampeleka nduguye Lemi klabuni na kucheza densi hadi che
 • Bi Kangara anamwingiza Sauna na Wengine katika biashara haramu ya kuwaiba Watoto na kuwauza.
 • Mwangemi na Mwangeka wananyimwa chakula na mama zao kama njia ya kuwaadhibu.
 • Wanawake wanafanya ukahaba na Tenge machoni pa Chandachema na Watoto wa Tenge.
 • Zohali anakataa kumfahamisha mwanawe Nasibu kwamba alikuwa na babu na nyanya.
 • Zohali aliwaua wazaziwe wakiwa hai kwa kudanganya kuwa walikufa miaka minane iliyopita.

Zozote 10×2=20

 1. Kigogo

 

 1. Ni maneno ya Majoka

Akimwambia Chopi

Katika hoteli ya Majoka and Majoka Modern Resort

Ilikuwa ni baada ya kupata habari za kifo cha Ngurumo                                    4×1=4

 1. Mnyanyasaji-anawatesa na kuwapiga wafungwa kwa amri ya majoka

Mfuasi kipofu-anaamrishwa na Majoka awaambie polisi wawafyatulie risasi na vitoza machozi waandamanaji.Anaendeleza maovu ya Majoka

Katili-anamdhuru Tunu kwa nia ya kumuua

Mpyaro-anatumia maneno makali kwa Sudi                                           3×2= 6

 • Ni kielelezo cha ukoloni mamboleo

Anawakilisha watumishi wa viongozi ambao wanaendeleza maovu ya viongozi kwa nia ya kujifaidi wenyewe/tamaa                                                             2×2=4

 1. Nahau-toa kafara-sadaka inayotolewa kwa lengo la kupata kinga dhidi ya mizimu

Kutaja, mfano                                                                                           2×1=2

 1. Anazungumzia kuua mtu mmoja ilhali anarejelea kuwepo kwa usalama katika jamii.

Wanazungumzia kuua mtu (kafara) ili kuleta mambo mema ilhali kifo cha mtu hakiwezi kuleta mema katika jamii                                                         2×2 =4


MWONGOZO WA INSHA

KIDATO CHA TATU 2019 MUHULA 2

 

Hii ni ripoti ya kawaida

Sura

 • Mada-ikionyesha kiini cha ripoti
 • Utangulizi -uwe na maelezo mafupi kuhusu lengo la kuandaa ripoti
 • Mwili-usheheni vijimada vidogo ambavyo vinabeba hoja kuu.
 • Tamati-iwe na jina la mwandishi wa ripoti na cheo chake.

Maudhui

 • Kuanzisha miradi ya kunyunyizia mashamba maji
 • Kulima mimea inayostahimili kiangazi
 • Kukusanya na kuhifadhi maji ya mvua
 • Kufuga Wanyama wanaostahimili kiangazi kama vile ngamia, punda, kuku
 • Upanzi wa mimea anuwai ili kuwa na mawanda mapana ya kupata chakula
 • Uhifadhi wa mazingira/ kupunguza uchafuzi wa mazingira
 • Kulinda chemichemi za maji na misitu
 • Kutenga sehemu za ujenzi ili watu wasikate miti ovyo.
 • Kulazimisha viwanda kuwajibika katika uhifadhi wa mazingira. n.k.

MWONGOZO WA KUDUMU

UTANGULIZI.

Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi,akizingatia mada aliyopewa. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kuikadiria kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivyopendekezwa. Viwango vyenyewe ni A, B, C na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa.

VIWANGO MBALIMBALI.

KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05.

 1. i) Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahinilazima afikirie kile mtahiniwa anachojaribu kuwasilisha.
 2. ii) Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.

iii) Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makosa ya kila aina.

 1. iv) Kujitungia swali na kulijibu.
 2. v) Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D.

D- (D YA CHINI) MAKI 01-02.

 1. i) Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.
 2. ii) Kujitungia swali tofauti na kulijibu.

iii) Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.

 1. iv) Kunakili swali au maswali na kuyakariri.
 2. v) Kunakili swali au kichwa tu.

D WASTANI MAKI 03.

 1. i) Mtiririko wa mawazo haupo.
 2. ii) Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.

iii) Matumizi ya lugha ni hafifu mno.

 1. iv) Kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (D YA JUU) MAKI 04-05.

 1. i) Insha ya aina hii hukuwa na makosa mengi ya kila aina, lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
 2. ii) Hoja hazikuelezwa kikamilifu/ mada haikukuzwa vilivyo.

iii) Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.

 1. iv) Mtahiniwa hujirudiarudia.
 2. v) Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.

KIWANGO CHA C KWA JUMLA MAKI 06-10.

 1. i) Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
 2. ii) Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia

iii) Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.

 1. iv) Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
 2. v) Insha ina makosa mengi ya sarufi, ya msamiati na ya tahajia (hijai).

C- (C YA CHINI) MAKI 06-07.

 1. i) Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
 2. ii) Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.

iii) Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi.

C WASTANI MAKI 08.

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
 2. i) Dhana tofauti tofauti hazijitokezi wazi.
 3. ii) Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.

iii) Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.

 1. iv) Anajaribu kushughulikia mada aliyopewa.
 2. v) Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
 3. vi) Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka.

 

C+ (C YA JUU) MAKI 09-10.

 1. i) Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
 2. ii) Dhana tofauti tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.

iii) Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.

 1. iv) Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
 2. v) Ana shida ya uakifishaji.
 3. vi) Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA MAKI 11-15

 1. i) Mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
 2. ii) Mtahiniwa anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.

iii) Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.

 1. iv) Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
 2. v) Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

Ngazi mbalimbali za kiwango cha B.

B- (B YA CHINI) MAKI 11-12

 1. i) Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti tofauti akizingatia mada.
 2. ii) Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.

iii) Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.

 1. iv) Makosa yanadhihirika kiasi.

B WASTANI MAKI 13

 1. i) Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
 2. ii) Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.

iii) Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.

 1. iv) Sarufi yake ni nzuri.
 2. v) Makosa ni machache/ kuna makosa machache.

B+ (B YA JUU) MAKI 14-15

 1. i) Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anajieleza waziwazi.
 2. ii) Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.

iii) Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.

 1. iv) Sarufi yake ni nzuri.
 2. v) Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
 3. vi) Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20

 1. i) Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
 2. ii) Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.

iii) Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.

 1. iv) Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo.
 2. v) Insha ina urefu kamili.

USAHIHISHAJI NA UTUNZAJI KWA JUMLA.

Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai.

MAUDHUI.

Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa. Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile. Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule.

MSAMIATI.

Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika. Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule. Kutegea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao.

MTINDO.

Mtindo unahusu mambo yafuatayo:

 • Mpangilio wa kazi kiaya.
 • Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.
 • Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.
 • Matumizi ya tamathali za usemi, kwa mfano methali, misemo, jazanda na kadhalika.
 • Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp, Uu, Ww na kadhalika.
 • Sura ya insha.
 • Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

SARUFI.

Sarufi ndio msingi wa lugha. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:

Matumizi ya alama za uakifishaji.

 1. Kutumia herufi kubwa na ndogo mahali pasipofaa.
 2. Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.
 3. Mpangilio wa maneno katika sentensi.
 4. Mnyambuliko wa vitenzi na majina.
 5. Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.
 6. Matumizi ya herufi kubwa katika:
 7. Mwanzo wa sentensi.
 8. Majina ya pekee.
 9. Majina ya mahali, miji, nchi, mataifa na kadhalika.
 10. Siku za juma, miezi n.k

iii. Mashirika, masomo,vitabu n.k

 1. Jina la mungu.
 2. Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa- Foksi, Jak, Popi, Simba,

Tomi na mengineyo.

MAKOSA YA HIJAI/TAHAJIA.

Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu.

Makosa ya tahajia huweza kutokea katika:

Kutenganisha neno kwa mfano ‗aliye kuwa‘

Kuunganisha maneno kwa mfano ‗kwasababu‘

Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile ‗ngan – o‘.

Kuandika herufi isiyofaa kwa mfano ‗ongesa‘ badala ya ‗ongeza‘

Kuacha herufi katika neno kwa mfano ‗aliekuja‘ badala ya ‗aliyekuja‘

Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile ‗piya‘ badala ya ‗pia‘

Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile j i

Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukosa kukiandikia mahali pasipofaa.

Kuacha ritifaa au kuiandikia mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe, ngom‘be, n‘gombe, ngo‘mbe n.k

Kuandika maneno kwa kifupi kama vile k.v, k.m, v.v, n.k na kadhalika.

Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2010.

UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA.

Maneno 9 katika kila mstari – ukurasa moja na nusu.

Maneno 8 katika kila mstari – ukurasa moja na robo tatu.

Maneno 7 katika kila mstari – kurasa mbili.

Maneno 6 katika kila mstari – kurasa mbili na nusu.

Maneno 5 katika kila mstari – ukurasa mbili na robo tatu.

Maneno 4 katika kila mstari – kurasa tatu na robo tatu.

Maneno 3 katika kila mstari – kurasa nne na nusu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top