• Sun. Oct 13th, 2024

Form 1 Kiswahili Exams and Marking Schemes Free

ByCitizen digital

Oct 9, 2024

Form 1 Kiswahili Exams and Marking Schemes Free

JINA:…………………………………………………. NAMBARI YA USAJILI……………

SHULE:……………………………………………………………………………………….. DARASA:……………

 

KISWAHILI

KIDATO CHA KWANZA

 

MUDA: SAA 2 ½

 

JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA

MUHULA WA TATU

MAAGIZO KWA MTAHINIWA

JIBU MASWALI YOTE

 

 

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI UPEO ALAMA
1.     UFAHAMU 15  
2.     SARUFI 40  
3.     ISIMU JAMII 10  
4.     FASIHI 15  
JUMLA 80  

 

 

  1. UFAHAMU (Alama 15)

Ulimwengu mzima ulisimama ghafla na shughuli za kawaida zikakwama katika mataifa yote duniani. Walimwengu walipata kibarua kigumu mno huku shughuli za uchukuzi wa kimataifa zikitatizika kwa njia zisizomithilika. Ikumbukwe pia kuwa masomo yalitatizika pakubwa huku viwango vyote vya shule vikifungwa.

 

Vituo vya afya navyo vilifurika kwa msongamano mkubwa wa watu huku wahudumu wa afya wakilemewa na idadi kubwa ya magonjwa. Wahudumu hao walijipata kwenye wadi na vyumba vya wagonjwa mahututi na wengine wengi walifariki. Wengineo walikosa nafasi ya matibabu au ya kulazwa katika hospitali wanazohudumu.

 

Uchumi uliathirika pakubwa. Watu wengi walipoteza kazi zao. Wengine walitumwa nyumbani kwa likizo bila malipo nao wengine wakikatwa mishahara kwa asilimia kubwa. Biashara nazo hazikusazwa na gonjwa hili kwani nyingi zilifungwa wengine wakipata hasara chungu nzima. Benki zilijipata kwa njia panda kwa wateja kushindwa kulipa mikopo.

 

Usisahau kuwa maelfu ya watu walipoteza maisha yao huku wengine wengi wakiendelea kukabiliana na makali ya ugonjwa wa Covid-19 ambayo kwa sasa ni uhakika kuwa umejua kuwa ndio ninaozungumzia. Kenya, kama mataifa mengine ulimwenguni inaendelea kukabiliana na janga hili.

 

Miongoni mwa dalili za mapema za maambukizi ya gonjwa hili ni kukohoa, kushindwa kupumua au ugumu wa kupumua, joto jingi au baridi kali mwilini, maumivu ya misuli au mwili, kutapika au kuendesha, kupoteza hisia za kuonja na kunusa miongoni mwa mengine. Yeyote anayeonyesha dalili hizi anashauriwa kujitenga na kwenda hospitalini mara moja.

 

Ni muhimu kujilinda dhidi ya virusi hivi. Vaa barakoa wakati unapoenda kwenye watu. Kumbuka kuosha mikono yako kwa maji yanayotiririka na sabuni au kutakasa. Epuka mikusanyiko ya watu na uzingatie umbali wa mita moja unapokumbana na watu. Kaa nyumbani kama inawezekana. Wenye magonjwa mengine kama shinikizo ya damu, ukimwi, saratani, kisukari miongoni na pia watu wa umri wa juu wanashauriwa na wataalamu wa afya wawe makini Zaidi kwani wamo hatarini Zaidi.

Hebu tugeukie mikakati mbalimbali iliyowekwa na serikali ya Kenya tangu kuliporipotiwa kisa cha kwanza nchini. Serikali ilitangaza kufungwa kwa shule. Kando na kufungwa huko, kafyu ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi iliwekwa hapo awali, hatua iliyolegezwa baadaye. Kufungwa kwa uchukuzi wa kimataifa ulitangazwa huku uchukuzi nchini ukidhibitiwa kwa kupunguzwa kwa idadi ya watu kwenye uchukuzi wa uma. Mikusanyiko ya watu ilipigwa marufuku nazo kanisa zikifungwa japo kwa muda. Idadi ya watu katika arusi na mazishi ilipunguzwa mno. Maeneo ya burudani pia yalifungwa kwa muda nayo maeneo ya maabadini yalifungwa miongoni mwa mikakati mingine

 

Baada ya miezi kadhaa makali ya janga hili tandavu yalizidi kuwakumba wakenya huku kufungwa kwa nchi kukiendelea kuathiri shughuli ya kawaida za kujikimu. Serikali iliweka mikatati ya kuinua uchumi. Wakenya wa viwango vya chini walitumiwa pesa za kujikimu huku wafanyibiashara wadogo wakiinuliwa kwa mikopo. Serikali pia ilizuia benki kuzungumza na madeni wao na kuwasongezea nyakati za kulipa. Ikumbukwe pia serikali ilipunguza ushuru kwa wakenya wenye kipato cha chini. Serikali pia ililazimika kulegeza mikakati kadhaa ili kuwapa wakenya nafasi ya kujichumia. Saa za kafyu zilipunguzwa huku uchukuzi wa kitaifa na kimataifa ukifunguliwa upya. Shule pia zilianza kufunguliwa japo kwa watahiniwa. Wamiliki wa maeneo ya burudani walinufaika na kufunguliwa kwa maeneo hayo.viongozi wa kidini na wafuasi wao walikuwa na kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuwafungulia maeneo ya kuabudu.

 

Wakenya wanaendelea kuhimizwa kufuata kanuni za wizara ya Afya dhidi ya Covid-19. Hii inaendelea huku wakenya wakilaumiwa kwa kutovaa barakoa, kuendelea kutangamana katika mikutano ya kisiasa, kutoosha wala kutakasa mikono, kutozingatia saa za kafyu miongoni mwa mengine.

Ulimwengu unaendeleza mchakato wa kutafiti na kutafuta chanjo ya korona huku baadhi ya mataifa wakitangaza kupiga hatua kubwa na kwamba tutakwamuliwa hivi karibuni. Kujilinda kunabaki kuwa chanjo kuu.

 

Maswali

  1. Nini kilisababisha ulimwengu kusimama ghafla.

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….                                                                                                                                                (al.1)

  1. Eleza kinaya kinachojitokeza kwa Covid-19 na wahudumu wa afya.             (al.1)

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

 

  1. Covid-19 imesababisha madhara mengi ya kiuchumi. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja tatu.             (al.3)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

 

  1. Taja dalili zozote mbili za maambukizi ya virusi vya korona.             (al.2)

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

  1. Eleza matendo matatu kulingana na kifungu hiki ambayo yanamweka mtu kwenye hatari ya maambukizi ya ugonjwa huu.             (al.3)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  1. Taja mikakati minne iliyowekwa na serikali ya Kenya kukabiliana na virusi hivi. (al.2)

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

  1. Serikali ya Kenya ililegeza mikakati yake vipi?             (al.1)

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

  1. Eleza maana ya maneno yafuaayo jinsi yalivyotumika kifunguni;             (al.2)
  2. Kafyu

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

  1. Mchakato

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  1. SARUFI (ALAMA 40)
  • a) Taja viyeyusho viwili.       (al.1)

……………………………………………………………………………………….

  1. b) Taja vipasuo viwili vya midomoni.       (al.1)

………………………………………………………………………………………..

  • Weka shadda katika maneno yafuatayo.                                                       (al.2)
  1. ua
  2. kumbukumbu
  • nafsi
  1. mwanafunzi
  • Onyesha aina za maneno katika sentensi zifuatazo.                               (al.4)

i.Walahi! Nikimuona Kamau nitampiga.

 

 

ii.Mimi nilimwambia jana asubuhi.

 

 

 

  • Taja matumizi mawili ya herufi kubwa na utolee mfano kwa kila matumizi. (al.4)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

  • Bainisha ngeli za maneno yafuatayo;                                                       (al.3)

sanduku –

rangi –

uteo –

  • Kanusha sentensi ifuatayo;                                                                   (al.2)

Mwalimu amekuwa akitufundisha.

………………………………………………………………………………………

  • Toa dhana ya vitate na utolee mfano.                                                       (al.2)

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

  • Andika kwa udogo.                                                                               (al.2)

Mtoto amevuka mto ule.

……………………………………………………………………………………….

  • Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.       (al.2)

Bibi yake ni mgonjwa.

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  • Onyesha viambishi awali na tamati katika neno lifuatalo       (al.2)

Amesomeshwa

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  • Bainisha hali na nyakati katika sentensi zifuatazo.       (al.4)

Mama ameenda shambani –

Nikimpata nitamwambia –

Mwalimu anafundisha –

Juma atafika kesho –

  • Andika maneno yafuatayo katika kauli uliyopewa.       (al.4)
  1. anika (tendua) –
  2. piga (tendana) –
  • soma (tendeshwa) –
  1. ogopa (tendesha) –
  • Tenga silabi katika maneno yafuatyo.       (al.2)
  1. nafsi –
  2. oa –
  • shukuru –
  1. kwao –
  • Andika kinyume cha sentensi ifuatayo;       (al.2)

Mwalimu mrefu ameketi chini.

………………………………………………………………………………………

  • Toa dhana ya kiimbo.       (al.1)

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  • Sentensi zifuatazo zinaleta dhana zipi za kiimbo.       (al.2)
  1. Juma alifika saa ngapi?

……………………………………………………………………………….

  1. Salale! Kumbe alikuwa mwizi.

………………………………………………………………………………..

 

  1. ISIMU JAMII ALAMA 10

Nanii kuku …? Sosi poa leo… mate ndo! Ndo! Ndo! Ukimanga hii hutaona daktari kwa miaka kumi… Ng’ombe je? Nani …. Nani? Ni wewe… poa basi naja…

 

  1. Hii ni sajili gani? Toa sababu.                                                                   (al.2)

……………………………………………………………………………………….

  1. Taja sifa sita za sajili uliotaja.                                                                   (al.6)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  • Kando na sajili uliyoitaja, tambua sajili zingine mbili za lugha.                   (al.2)

…………………………………………………………………………………………………………………….

……………………………………………………………………………………….

  1. FASIHI SIMULIZI ALAMA 15
  • Toa dhana ya maneno yafuatayo.             (al.3)
  1. Hadhira

………………………………………………………………………………………

  1. Fasihi

………………………………………………………………………………………

  • Ngano

………………………………………………………………………………………

  • Taja aina mbili za fasihi.             (al.2)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  • Taja aina nne za nyimbo.                                                             (al.4)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

  • Eleza umuhimu wa fasihi katika jamii.             (al.6)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

_________________________________________________________________________________________________

MUHULA WA TATU

KIDATO CHA KWANZA

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 

UFAHAMU

  1. Ugonjwa wa Covid-19 na makali yake (1×1)
  2. Wanahudumu wa afya walikosa nafasi ya matibabu au nafasi ya kulazwa katika hospitali wanazohudumu wenyewe.     (1×1)
  3. – Watu wengi kupoteza kazi zao.
  • Watu wengine kutumwa kwa likizo bila malipo.
  • Wengine kukatwa mishahara kwa asilimia kubwa.
  • Biashara nyingi kufungwa nyingi zikipata hasara chungu nzima.
  • Benki kuathirika kwa wateja kushindwa kulipa mikopo.   (3×1)
  1. -Kukohoa
  • Kushindwa kupumua au ugumu wa kupumua.
  • Joto jingi au baridi kali mwilini.
  • Maumivu ya misuli au mwili.
  • Kutapika au kuendsha, kupoteza hisia za kuonja na kunusa.   (2×1)
  1. – Kutovaa barakoa kila wakati unapoenda kwenye watu.
  • Kutoosha mikono yako kwa maji yanayotirirka na sabini au kuitakasa.
  • Kwenda kwenye mikusanyiko ya watu.
  • Kutozingatia umbali wa mita moja unapokumbana na watu.   (3×1)
  1. – Serikali ilitangaza kufungwa kwa shule.
  • Kafyu ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi iliwekwa hapo awali.
  • Kufungwa kwa uchukuzi wa kimataifa ulitangazwa.
  • Kudhibitiwa kwa uchukuzi nchini kwa kupunguzwa kwa idadi ya watu kwenye uchukuzi wa uma.
  • Mikusanyiko ya watu ilipigwa marufuku.
  • Kanisa kufungwa japo kwa muda.
  • Idadi ya watu katika arusi na mazishi kupunguzwa mno.
  • Maeneo ya burudani pia yalifungwa kwa muda.   (4×1/2)
  1. – Saa za kafyu zilipunguzwa.
  • Uchukuzi wa kitaifa na kimataifa ulifunguliwa upya.
  • Shule pia zilianza kufunguliwa japo kwa watahiniwa.
  • Kufunguliwa kwa maeneo ya burudani.
  • Maeneo ya kuabudu yalifunguliwa japo kwa masharti ya kiafya.   (2×1/2)
  1. i) Kafyu- Amri ya kutotoka nje nyakati fulani kama vile usiku hadi asubuhi. (1×1)
  2. ii) Mchakato –Hatua za kufuata wakati wa kufanya jambo                        (1×1)

 

SARUFI ( alama 40)

  1. a) /w/, /y/ (1×1/2)
  2. b) /p/, /b/ (1×1/2)
  3. i) ‘ua
  4. ii) kumbu‘kumbu

iii) ‘nafsi

  1. iv) mwana‘funzi (1×1/2)
  2. walahi- kihisishi (I)

nilimuona kitenzi (T)

Kamau –nomino  (N)

nitampiga – kitenzi (T)    (4×1/2)

 

ii.mimi – kiwakilishi (W)

nilimwambia –kitenzi ( T)

jana – kielezi (E)

asubuhi – kielezi (E)       (4×1/2)

  1. Mwanzoni mwa sentensi mf. Mwalimu ameingia darasani.

Kuandika nomino za pekee mf. Kenya, Tana, Juma.

(Majina ya watu, milima, mito, miji, nchi, mwezi, siku)    (matumizi alama mbili mifano alama mbili)

  1. Sanduku LI-YA

Rangi        I-I

Uteo          U-ZI      (3×1)

  1. Mwalimu hajakuwa akitufundisha. (2×1)
  2. vitate ni maneno yanayotatanisha kimatamshi.

Mfano. Paa  baa  bata  pata (Maana alama moja,mfano alama moja)

  1. Kitoto/kijitoto kimevuka kijito kile. (2×1)
  2. Mke wake ni mgonjwa.

Nyanya yake ni mgonjwa.    (2×1)

  1. Ame- viambishi awali

eshwa – viambishi tamati     (2×1)

  1. Hali timilifu

‘ki’ ya masharti

Wakati uliopo

Wakati ujao      (4×1)

  1. i) anua
  2. ii) pigana

iii)someshwa

iv)ogofya        (4×1)

  1. Naf-si

o-a

shu-ku-ru

kwa-o       (2×1)

  1. Mwalimu mfupi amesimama juu. (2×1)
  2. Kiimbo ni kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti mtu anapozungumza. (1×1)
  3. i) Swali
  4. ii) Mshangao (2×1)

ISIMU JAMII

  1. sajili ya hotelini/mkahawani. (Kutaja alama moja sababu alama moja)

 

  1. matumizi ya msamiati maalum mf. Karanga, sosi

matumizi ya misimu mf. Ukimanga

matumizi ya tanakali za sauti mf. Mate ndo!ndo!ndo!

matumizi ya sentensi fupifupi

lugha ya ucheshi na utani

kuchanganya ndimi

lugha si sanifu.  ( Kutaja ½ mfano alama ½)

 

  • sajili ya uwanjani

sajili ya darasani

sajili ya kanisani.    (2×1)( mwalimi akadilie jibu la mwanafunzi)

FASHI SIMULIZI (ALAMA 15)

  1. hadhira- ni wasikilizaji au watazamaji wa kazi yoyote ya fasihi.

Fasihi – ni Sanaa inayotumia lugha kwa ufundi kuwasilisha ujumbe kwa mwanadamu.

Ngano – hivi ni visa vya kubuni au vya kweli ambavyo huwasilishwa kwa lugha kinathari kuhusu watu, matukio na mahali mbalimbali.    (3×1)

  1. Fasihi simulizi

Fasihi andishi      (2×1)

  1. Nyimbo za siasa

Bembea/bembelezi/pembelezi

Nyimbo za kazi/hodiya

Nyimbo za watoto (chekechea)

Nyiso

Nyimbo za sifa (sifa)

Nyimbo za mapenzi.    (4×1)

  1. Kuhifadhi na kuridhisha maarifa ya jamii.

Husaidia kukuza lugha

Fasihi hupumzisha (huburudisha na huliwaza)

Fasihi ni kitambulisho cha jamii za binadamu

Husaidia kukuza au kujonga tabia

Kumburudisha na kumstarehesha binadamu

Kuichochua na kuelimisha jamii

Huadilisha/kukuza maadili

Huunganisha na kuibua hisia za mzalendo.    (6×1)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *