FASIHI SIMULIZI NOTES FORM 1-4 IN PDF FREE

FASIHI SIMULIZI

Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu.

Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na hisia za binadamu kama vile maneno, maandishi, uchoraji, uchongaji, ufinyanzi n.k.

DOWNLOAD FREE PDF NOTES HERE; Free Kiswahili Fasihi notes, Ushairi notes, isimu Jamii notes and Many More: Mwongozo wa kigogo, Kidagaa, Tumbo lisiloshiba, Chozi..

Fasihi simulizi ni sanaa kwa vile:

  1. Huwasilisha ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumi.
  2. Huwa na umbo mahsusi k.m. hadithi huwa na mwanzo, kati na mwisho na mashairi huwa na beti, mishororo, n.k.
  3. Hutumia lugha kwa ufundi k.v. ya kitamathali.
  4. Husawiri mandhari/mazingira mahsusi kwa ufundi mkubwa.
  5. Hujenga wahusika kwa ustadi mkuu ili kusawiri tabia za watu katika jamii.

Tofauti Kati ya Fasihi na Sanaa Nyingine

fasihi sanaa nyingine
ü  Kutumia lugha

ü  Sanaa tendi

ü  Kutumia wahusika kuwasilisha maudhui

ü  Kutumia maudhui na fani kuwasilisha ujumbe

ü  Kujikita katika mazingira na wakati maalum

ü  Kutotumia lugha

ü  Si tendi

ü  Hutumia maumbo kumithilisha watu

ü  Kutumia maumbo na sura za vitu

 

 

ü  Hazijikiti katika muktadha na wakati maalum.

Aina/makundi ya fasihi

  1. Fasihi simulizi
  • Fasihi inayowasiolishwa kwa njia ya mdomo.
  1. Fasihi andishi
  • Fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi.

Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi/sifa za fasihi simulizi/zinazofanya utanzu uwe wa fasihi simulizi

  1. Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
  2. Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi.
  3. Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi.
  4. Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.
  5. Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi.
  6. Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira.
  7. Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira.
  8. Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum.
  9. Fasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi haiandamani na shughuli ya kitamaduni.
  10. Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi, maigambo.
  11. Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya.
  12. Fasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamu
  13. Fasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalum.
    • Tofauti kati ya hadhira
  14. Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi simulizi sio lazima iwasiliane na mwandishi.
  15. Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi k.v kwa kuimba, kupiga makofi n.k (hadhira tendi/hai) ilhali hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi.
  16. Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi.
  17. Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile ya fasihi andishi kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika.
  18. Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani ilhali ile ya fasihi simulizi si hai yaani haijulikani na mwandishi.
  19. Hadhira ya fasihi simulizi hainunui kazi ilhali ile ya fasihi andishi hununua kazi.
  20. Hadhira ya fasihi simulizi yaweza kumiliki kazi ya fanani lakini ile ya fasihi andishi haiwezi kumiliki kazi ya mwandishi.
  21. Hadhira ya fasihi simulizi huchagua kwa kulenga watu wa rika fulani lakini ile ya fasihi andishi hailengi watu wa rika yoyote.

Jinsi Fasihi Simulizi na Andishi Zinavyofanana

  1. Zote mbili hushughulikia masuala yanayohusu maisha maisha ya binadamu.
  2. Zote mbili Huhumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha maudhui.
  3. Zote mbili huwa na vipengele viwili vikuu, maudhui na fani (jumla ya mbinu msanii alizotumia kuwasilisha maudhui).
  4. Zote mbili majukumu sawa k.v. kuburudisha, kuadilisha, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni, n.k.
  5. Zote mbili zina utendaji-pale tamthilia na riwaya zinapoigizwa.
  6. Zote mbili huzaliwa, hukua na hufa kutegemea mabadiliko ya wakati.
  7. Zote mbili huwa na wawasilishaji-fanani k.m. mtambaji/mganaji au manju/yeli katika fasihi simulizi na mwandishi upande wa fasihi andishi .
  8. Fasihi simulizi imekopa tanzu za fasihi simulizi k.v. methali, mashairi, n.k.

Majukumu ya Fasihi Simulizi/Umuhimu wa Kufunza Fasihi Simulizi Katika          Shule za Upili

  1. Kuburudisha-kustarehesha, kufurahisha, kuchangamsha, kutuliza, kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili – nyimbo, hadithi, vitendawili
  2. Kufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na kukataa sifa hasi za wahusika.
  3. Kukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo.
  4. Kufariji k.m mbolezi na methali k.m. ‘Baada ya dhiki faraja’.
  5. Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi wa fasihi andishi.
  6. Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k.
  7. Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k.
  8. Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ – Mtu hawezi kumwoa dadake.
  9. Kuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k.
  10. Kukuza lugha k.v. misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha sanifu.
  11. Kukuza uwezo wa kutumia lugha kadiri mtu anapoendelea kuwasilisha k.v. hotuba, vitanza ndimi husaidia kuboresha matamshi na kutofautisha maana za maneno.
  12. Kuza uwezo wa kubuni k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k.
  13. Kukuza uzalendo kwa kufanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa au watu waliotendea jamii makuu.
  14. Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k.

Sababu za Ufaraguzi/Kubadilika kwa Fasihi Simulizi

  1. Kuwasilishwa vibaya.
  2. Fanani kusahau na kubadilisha yaliyomo na mtiririko.
  3. Kubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira k.m. umri na uelewa wao- kutumia lugha nyepesi kwa watoto na pevu kwa watu wazima.
  4. Mabadiliko ya mandhari/mazingira-vitu vilivyo katika mazingira halisi kukosekana katika mazingira ya usimulizi na msimulizi kutumia vitu katika mazingira yake vinavyokaribiana navyo.
  5. Kutoeleweka na hivyo kuhifadhiwa vibaya.
  6. Mabadiliko ya wakati k.m kitendawili cha wakati wa mkoloni kutumia mzungu na cha wakati wa mwarabu kutumia mwarabu na maana ni ile ile-Mzungu/mwarabu amesimama kwa mguu mmoja-mwavuli.
  7. Mabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale ambayo ni muhimu na kuacha mengine.
  8. Kila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha/kisanii.
  9. Ubunifu wa fanani ili uwasilishaji uweze kuvutia saidi na uwezo wake wa lugha.
  10. Teknolojia kusababisha kuhifadhiwa na hivyo kuiua.

Wahusika katika Fasihi Simulizi

  • Wahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali.
  1. Fanani-anayetunga na kuwasilisha fasihi simulizi.
  2. Hadhira-kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira: (i) hadhira tendi/hai na (ii) hadhira tuli.
  3. Wanyama-wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tu.
  4. Binadamu
  5. Mazimwi na majitu-viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu ananyoyapendeza.
  6. Wahusika vitu (visivyo na uhai) mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa kuibua imani za kidini.
  7. Mizimu-roho za waliokufa-hutembea, hula na huathiri binadamu.
  8. Miungu-viumbe vyenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika mighani na visasili.

Njia za Kukusanya Fasihi Simulizi

  1. Kuchunza/utazamaji
  • Kutazama kwa makini yanayotokea na kuandika.

Umuhimu/ubora/uzuri

  1. Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.
  2. Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
  3. Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika
  4. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
  5. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji

Udhaifu

  1. Shida ya mawasiliano.
  2. Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kumshuku na kusitisha uwasilishaji
  3. Ghali kwa kumbidi mtafiti kusafiri
  4. huhitaji muda mrefu
  1. Kusikiliza wasanii wakiwasilisha tungo zao.

Umuhimu

  1. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
  2. Kupata habari za kutegemewa na kuaminika.
  3. Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
  4. Kikwazo cha mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  5. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji.

Udhaifu

  1. Shida ya mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  2. Huhitaji muda mrefu-kusafiri na kusikiliza.
  3. Ugeni wa mtafiti kusababisha washiriki kutowasilisha ipasavyo.
  4. Ghali kwa gharama ya usafiri.
  1. Mahojiano
    • Kuhoji wanaofahamu mengi kuhusu fasihi simulizi.

Umuhimu                                                                                          

  1. Kuweza kung’amua wakati mhojiwa anatoa habari zisizo za kweli.
  2. Kuweza kufafanulia mhojiwa maswali ili kuweza kupata habari sahihi zaidi.
  3. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.
  4. Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.
  5. Kupata habari za kutegewa na kuaminika

Udhaifu

  1. Huhitaji muda mrefu.
  2. Mhojiwa kutotoa habari kwa kutomwamini mtafiti kwa ugeni wake.
  3. Kikwazo cha mawasiliano-si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  4. Ghali kwa gharama ya usafiri.
  1. Kurekodi katika kanda za sauti/tepurekoda

Umuhimu

  1. Kuweza kudumu na kufikia vizazi vingi.
  2. Sifa za uwasilishaji/uhai kama vile toni na kiimbo kuhifadhiwa.
  3. Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa.
  4. Kupata habari za kutegewa na kuaminika
  5. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji

Udhaifu

  1. Chaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
  2. Hakiwezi kunasa uigizaji.
  3. Fanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwa.
  4. Ghali kwa kuhitaji kununua kifaa na kumbidi mtafiti kusafiri.
  1. Kurekodi kwa filamu na video
    • Hunasa picha zenye miondoko na sauti.

Umuhimu

  1. Video huhifadhi uigizaji, ishara na kiimbo/toni.
  2. Kuonyesha uhalisi wa mandhari
  3. Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa
  4. Kazi iliyokusanywa hivi hudumu kwa muda mrefu.
  5. Njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika
  6. Kupata habari za kutegewa na kuaminika

Udhaifu

  1. Chombo chaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
  2. Fanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwa.
  3. Njia ghali.
  4. Fanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwa.
  5. Ghali kwa gharama ya ya usafiri na kununua filamu na kamera ya video.
  6. Data yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwa.
  7. f) Kupiga picha kwa kamera
    • Hunasa picha zisizo na miondoko na sauti

Umuhimu

  1. Huonyesha uhalisi wa mandhari.
  2. Huweza kuhifadhi ishara.
  3. Mkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewa.
  4. Kupata habari za kuaminiwa na kutegemeka.

Udhaifu

  1. Ghali kwa gharama ya ya usafiri na kununua kamera.
  2. Sifa za uhai kama vile kiimbo haziwezi kuhifadhiwa.
  3. Yaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirika.
  4. Data yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwa
  1. Kushiriki katika kazi ya fasihi simulizi k.v. ngoma, soga, n.k.

Umuhimu

  1. Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishaji.
  2. Kupata habari za kutegewa na kuaminika.
  3. Njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  4. Kukuza utangamano wa mtafiti na wanajamii.
  5. Kuweza kunasa na kuhifadhi sifa za kiimbo, toni na ishara.

Udhaifu

  1. Kuchukua muda mrefu.
  2. Ugeni wa msanii kusababisha washiriki kuwa na wasiwasi na kutotenda kama kawaida.
  3. Njia ghali kwa kuhitaji mtafiti kusafiri mbali.
  4. Mtafiti aweza kusahau kwa kuhifadhi akilini.
  1. Kutumia hojaji
  • Fomu yenye maswali funge au wazi.

Umuhimu

  1. Gharama ya chini.
  2. Yaweza kutumika katika mahojiano.
  3. Huokoa muda kwani mtafiti aweza kuituma na kuachia mhojiwa kujaza.
  4. Hupatia habari za kuaminika na kutegemeka.

Udhaifu

  1. Utata wa maswali kusababisha majibu yasiyo sahihi.
  2. Si nzuri kwa wasiojua kusoma na kuandika.
  3. Kutopata sifa za uwasilishaji kama vile kiimbo, toni na ishara.
  4. Wahojiwa kukataa kuijaza kutokana na mwelekeo hasi dhidhi ya hojaji na hivyo kukwamiza utafiti.

Vifaa vya Kukusanya Fasihi Simulizi na Udhaifu Wake

  1. Vinasa sauti/tepu rekoda
  2. Kamera
  3. Filamu na video
  4. Diski za kompyuta
  5. Kalamu na karatasi

Umuhimu

  1. Kuweza kudumu na kufikia vizazi vingi.
  2. Si rahisi kusahaulika-hubakia vile vile.
  3. Si njia ghali kama vile video

Udhaifu

  1. Sifa za uwasilishaji kama vile toni, kiimbo/toni na ishara haziwezi kuhifadhika hivyo kupotea.
  2. Hupunguza hadhira kwa kulenga tu wanaojua kusoma na kuandika na hivyo kuathiri usambazaji wake.

Mbinu za Kuhifadhi Fasihi Simulizi

  1. Huhifadhiwa na binadamu akilini k.m. ngano hupokewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
  2. Katika maumbile au mazingira k.m. fisi daima huchechemea , kinyonga naye hutembea pole pole.
  3. Katika vifaa meme k.m. nyimbo, hadithi, maigizo n.k. huweza kuhifadhiwa katika kanda za sauti, video, sidi na diski za kompyuta.
  4. Katika michoro k.m. picha huhifadhi matukio maalum k.v. za kabila fulani likiwinda au likisherehekea.

Umuhimu wa Kukusanya/Kuhifadhi Fasihi Simulizi

  1. Ili isipotee k.m. kwa kusahaulika.
  2. Kuirekodi ili kuiendeleza kwa kuirithisha kwa vizazi vijavyo.
  3. Ili kulinganisha fasihi simulizi za jamii mbalimbali na kuonyesha tofauti zake.
  4. Ili kuhakikisha mtiririko katika uwasilishaji.
  5. Kutunza historia ya jamii ili vizazi vijavyo viijue.
  6. Ili kuziba mapengo ya utafiti yaliyomo kwa vile kuna tungo ambazo hazijatafitiwa kwa kina.
  7. Kuendeleza elimu ya jadi ya jamii.
  8. Kuingiliana na jamii iliyo chanzo cha fasihi humwezesha kuelewa na utamaduni na fasihi yake kwa ujumla
  9. Humwezesha mwanafunzi kuona vipengele hai vya fasihi k.v. uigizaji, toni na kiimbo ambavyo husaidia kuielewa kwa kina.
  10. Husaidia kuhifadhi tamaduni za jamii kwa nia ya kuzipitisha kwa vizazi vijavyo.
  11. Husaidia kuelewa utamaduni wa jamii nyingine.
  12. Humwezesha mwanafunzi kupata maarifa ya kufanya utafiti katika taaluma nyingine k.v. sosholojia.
  13. Kujua fasihi simulizi za jamii nyingine humfanya mtafiti kuzielewa na kuzikubali jamii hizo na hivyo kuendeleza amani katika nchi.
  14. Ili kusahihisha mawazo mapotovu kuhusu baadhi ya tanzu na vipera vya fasihi simulizi.

Matatizo Yanayomkabili Mkusanyaji wa Fasihi Simulizi

  1. Gharama ya utafiti kuwa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu k.v. kusafiria, kununulia vifaa.
  2. Kutojaziwa hojaji kutokana na mtazamo hasi wa jamii dhidi ya ujazaji wake.
  3. Wanajamii kukataa kutoa habari wakishuku mtafiti anawapeleleza au kwa kuona haya.
  4. Wanajamii wengine kudai walipwe kabla ya kutoa habari na hivyo kukwamiza utafiti.
  5. Mbinu nyingine k.v. hojaji huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika na ikiwa mhojiwa hajui utafiti utakwamizwa.
  6. Uchache wa wazee na wataalamu wa fasihi simulizi kusababisha kukosekana au kupatikana kwa data isiyo ya kutegemewa.
  7. Utawala kukataa kutoa idhini ya kufanya utafiti.
  8. Kukosa ufadhili na utafiti kutofanywa kwa kutomudu gharama.
  9. Muda wa utafiti kutotosha na hivyo kutopata habari za kutosha kuhusiana na mada yake.
  10. Kikwazo cha mawasiliano ikiwa mtafiti na mhojiwa hawatumii lugha moja na mhojiwa hajui lugha nyingine na kumbidi mtafiti kukodi mkalimani na gharama kuongezeka.
  11. Ukosefu wa vyombo vya usafiri kunakochelewesha utafiti na kutomalizika katika muda uliopangwa.
  12. Ukosefu wa usalama k.v. kuvamiwa kwa kushukiwa anapeleleza na kuibiwa vifaa.

Changamoto Zinazokabili Ukusanyaji wa Fasihi Simulizi

  1. Ukosefu wa utafiti wa kutosha kwani kuna vipera ambavyo bado havijaandikwa.
  2. Uchache wa wataalamu wa kutafitia na kuendeleza utafiti.
  3. Watu kuhamia mijini na kuingiliana na wa jamii nyingine na kufanya uhifadhi na urithishaji wa fasihi kutowezekana.
  4. Mtaala wa elimu kupuuza lugha ya kiasili inayotumiwa kuhifadhia na kurithisha fasihi simulizi na hivyo kukatiza ukuaji wake.
  5. Fasihi simulizi kuhusishwa na ukale na hivyo kutoona haja ya kuirithisha na kuihifadhi.
  6. Kuhifadhiwa kwa fasihi simulizi akilini kusababisha kusahaulika, kubadilika hata kufa kwake.

Jinsi Jamii ya Sasa Inavyojaribu Kuhifadhi Fasihi Simulizi

  1. Tamasha za muziziki kunakokaririwa na kuimbwa mashairi.
  2. Sherehe za arusi, jando, mazishi mawaida.
  3. Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia redio na runinga.
  4. Sarakasi za wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho.
  5. Ngoma za kienyeji kama isukuti katika hafla za kisiasa na harusi.
  6. Utambaji wa hadithi hasa katika sehemu za mashambani.

Tanzu za Fasihi Simulizi

  • Tanzu ni aina za tungo zenye muundo uliokaribia kufanana.
  1. hadithi
  2. semi
  3. ushairi
  4. mazungumzo
  5. maigizo
  • Kipera ni utungo wa fasihi simulizi unaowasilishwa mbele ya watu.

HADITHI

  • Masimulizi yanayotumia lugha ya mtiririko au nathari.

Sifa

  1. Hutumia ya lugha ya mtiririko au nathari-kueleza matukio moja kwa moja.
  2. Hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
  3. Huwasilishwa mbele ya hadhira
  4. Hutambwa mahali maalum k.v. ndani ya nyumba, chini ya mti, uwanjani, n.k.
  5. Huweza kutokana na matukio halisi (kihistoria) au ya kubuni.
  6. Huwa na mafunzo fulani kwa jamii/hadhira.
  7. Hutumia wahusika wa aina tofauti k.v. nyumbani, wanyama, ndege, mazimwi, n.k.
  8. Hutumia aina nyingine za sanaa k.v nyimbo, methali, ushairi, n.k.
  9. Huwa na utendaji k.v. mtambaji kuiga fisi anavyokula.
  10. Aghalabu hutambwa jioni.

Sababu za Ngano Kutambwa Jioni/Usiku

  1. Ndio wakati watu walikuwa wamejumuika nyumbani baada ya kazi.
  2. Utambaji ulikuwa njia ya kupitisha wakati chakula kikingojewa.
  3. Wakati huu ulihakikisha mwanajamii hapotezi wakati wa kazi.

Majukumu ya Hadithi

  1. Kufunza maadili yaliyo nguzo kuu kwa wanajamii.
  2. Kukuza ujasiri wa kuzungumza hadharani.
  3. Kuburudisha baada ya kazi ya kutwa.
  4. Kukuza uwezo wa watoto wa kukumbuka ili kutamba baadaye.
  5. Kueleza asili ya mambo k.m visaviini, visasili na ngano za usuli.
  6. Kutahadharisha wanajamii dhidi ya kufanya mambo yasitofaa.
  7. Kuunganisha watu katika jamii wanapojumuika pamoja kusikiliza utambaji.
  8. Ngano za mtanziko hukuza uwezo wa kutathmini na kutoa uamuzi ufaao.
  9. Kukuza lugha hasa kwa hadhira ya watoto.
  10. Kuhifadhi na kuendeleza historia ya jamii k.v. mighani, tarihi, n.k.
  11. Kuelimisha hadhira kuhusu utamaduni wao.
  12. Njia ya kupokeza kizazi historia na utamaduni wa jamii.

Sifa za Mtambaji/Mganaji Bora

  1. Asiwe mwoga ili kuweza kuzungumza hadharani.
  2. Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidi.
  3. Awe na uelewa wa mazingira na masuala ibuka katika jamii ili kuweza kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake k.m. kutumia rais kuelezea dhana ya mfalme.
  4. Awe na ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha kwa wepesi.
  5. Awe mchanganfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai.
  6. Awe na ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhira.
  7. Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kuimba, maswali ya balagha ili isikinai, n.k.
  8. Aweze kujua, matarajio, kiwango cha elimu na tajriba ya hadhira ili kuweza kubadilisha kwa kiwango kinachofaa.
  9. Awe na uwezo wa kuingiliana vizuri na hadhira ili aivutie.
  10. Awe na kumbukumbu nzuri ili usimulizi wake utiririke vizuri.
  11. Awe na uwezo wa kudramatisha ili kuonyesha picha fulani k.v. kuiga toni, sauti, na kiimbo kulingana na swala analowasilisha.
  12. Kubadilisha toni au kiimbo ili hadhira isikinai.
  13. Awe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kulingana na hali anayoigiza.
  14. Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
  15. Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza k.v. huzuni
  16. Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa nyimbo na maswali ya balagha ili kuondoa uchovu wa kutazama na kusikiliza.
  17. Awe na uwezo wa ufaraguzi/ kubadilisha utambaji wake papo hapo kutegemea hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira.
  18. Awe na uwezo wa kutumia mtuo wa kidrama ili kuongeza taharuki, kusisitiza ujumbe na kuteka makini ya hadhira.

Aina za Hadithi

  1. Hadithi za Kubuni
  • Hazisimulii matukio ya kweli bali ya kutungwa
    1. Hadithi za Kisalua/Kihistoria
      • Zinazosimulia matukio yaliyowahi kutendwa na wahusika waliowahi kuishi.
      • Huongezewa ubunifu ili kuvutia zaidi.
        1. Hadithi za Kubuni

Ngano

  • Hadithi zinazosimulia kisa chenye funzo na zenye wahusika aina ya binadamu, viumbe na vitu visivyo na uhai.

Sifa za Ngano

  1. Zina fomyula ya kuanzia/mwanzo maalum.
  2. Zina fomyula ya kumalizia/mwisho maalum.
  3. Zina wahusika aina mbalimbali.
  4. Zina matumizi ya nyimbo.
  5. Hutumia takriri (usambamba) ili kusisitiza k.m. zimwi likakimbia, likakimbia.
  6. Huwa na na maadili/mafunzo
  7. Hutumia maswali ya balagha kuongeza taharuki.
  8. Hutumia tanakali za sauti.
  9. Zina matumizi ya fantasia au matukio yanayokiuka uhalisi/mambo ya ajabu k.v. binadamu kuruka kama ndege, zimwi kumeza watu na baadaye kutapika wote, n.k.
  • Kutambua mbinu zilizotumiwa katika hadithi/ngano
  • Kutambua wahusika

Aina za Fomyula za Kuanzia/Mianzo Maalum

  1. Paukwa, Pakawa. Sahani. Ya mchele. Giza. La mwizi. Na kiboko je? Cha mtoto mrorofi…
  2. Hapo zamani za kale/za kongamawe…
  • Ilitokea…
  1. Hadithi! Hadithi! Hadithi njoo…
  2. Kaondokea chenjangaa, kajenga nyumba kakaa, mwanangu mwanasiti, kijino kama chikichi, cha kujengea kikuta, na vilango vya kupita…
  3. Hapo jadi na jadudi…

Umuhimu wa Fomyula ya Kuanzia/Mwanzo maalum

  1. Kuvuta makini ya hadhira.
  2. Kumtambulisha mtambaji kwa hadhira.
  • Kuashiria mwanzo wa hadithi.
  1. Kutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi ule wa hadithi.

Aina za Fomyula za Kumalizia/Miishio Maalum

  1. Hadithi inaishia hapo.
  • Tangu siku hiyo…
  1. Wakaishi raha mustarehe.
  2. Maadili

Umuhimu wa Fomyula ya Kumalizia/Mwisho Maalum

  1. Kuashiria mwisho wa hadithi.
  2. Kutoa hadhira katika ulimwengu wa hadithi hadi ule halisi.
  • Kumpisha/kumpa fursa mtambaji anayefuata.
  1. Kupisha shughuli inayofuata.
  2. Kutoa funzo la hadithi kwa muhtasari.
  3. Kupa hadhira nafasi ya kupumzika baada ya kuwa makini kwa muda.

Umuhimu wa Nyimbo katika Ngano

  1. Kushirikisha hadhira.
  2. Kusisimua hadhira na kuondoa ukinaifu
  • Kuteka makini yao.
  1. Kuwasilisha mafunzo/maadili.
  2. Kutenganisha matukio katika hadithi.
  3. Kuburudisha hadhira.
  • Kupunguzia hadhira mwemeo.

Umuhimu wa Tanakali za Sauti/Onomatopeya katika Ngano

  1. Kuongeza utamu.
  2. Kusaidia msomaji kupata picha kamili.
  • Kusaidia kupata hisia halisi

Aina za Ngano

  1. Hurafa
  • Hadithi zenye wahusika wanyama na ndege.
  • Hurafa za kijanja ni hadithi ambapo wanyama wadogo hutumia ujanja wa hali ya juu ili kujinasua na hali ngumu au mitego wanayotegewa.

Sifa

  1. Wahusika ni wanyama au na au ndege.
  2. Wanyama na ndege hupewa sifa za binadamu
  3. Ni kazi ya ubunifu.
  4. Hutoa mafunzo kwa njia ya kuchekesha na isiyoumiza.
  5. Huwa na ucheshi mwingi.
  6. Hutumia mbinu ya uhuishi.
  7. Huwa na sifa zinazohimizwa na zinazoshutumiwa.
  8. Ujanja au uongo hujitokeza katika hurafa za kijanja.
  9. Ushindi hujitokeza katika hurafa za kijanja.

Umuhimu

  1. Kutahadharisha watu dhidi ya kuwa wa danganyifu/kudanganyika kwa urahisi.
  2. Kuonyesha jinsi tabia ya udanganyifu inavyoweza kujitokeza na kuathiri watu.
  3. Hurafa za kijanja hufunza jinsi ya kupampana na hali ngumu.
    1. Hekaya/Ngano za Kiayari
  • Hadithi zinazomsawiri mhusika anayetumia ulaghai kupata matilaba yake kutoka kwa wengine (Abunuwasi).

Sifa

  1. Wahusika wakuu ni binadamu.
  2. Huwa na ubunifu mkubwa.
  3. Hustaajabisha na kuchekesha.
  4. Ujanja na uongo hujitokeza.
  5. Ushindi hujitokeza.
  6. Ni za kubuni.

Umuhimu

  1. Hutahadharisha watu dhidi ya kuhadaika kwa wepesi.
  2. Huonya dhidi ya matokeo yanayoweza kuwapata wanaojinyakulia mali kwa udanganyifu.
  3. Kuonya dhidi ya usaliti.
  4. Kukashifu viongozi dhalimu na matendo maovu.
  5. Kukejeli wanaotumia nguvu badala ya akili/hekima.
    • Visasili
  • Hadithi zinazoeleza asili ya matukio fulani katika jamii k.m. kifo, jua, lugha, zilizala n.k.

Sifa

  1. Husimulia mambo ya kiimani na kidini.
  2. Huwa na misingi ya kihistoria.
  3. Hueleza asili ya matukio katika jamii.
  4. Wahusika ni wanyama na binadamu.
  5. Huwa na maadili.
  6. Hurithishwa kizazi hadi kingine.

Umuhimu

  1. Kueleza asili ya mambo kama vile kifo, utamaduni n.k.
  2. Kueleza utaratibu wa kutekeleza desturi k.v. mahari.
  3. Kuhalalisha baadhi ya mila na desturi za jamii k.v. ulipaji mahari, uabudu miti, n.k.
  4. Kukitisha mizizi imani fulani ya watu.
  5. Kupunguza athari za majanga kama vile kuhalalisha kifo.
  6. Kutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya visasili.
  7. Kuhifadhi historia na utamaduni wa jamii
    1. Ngano za usuli
  • Hadithi zinazoeleza asili ya hali, tabia, mahusiano au wasifu. k.v. asili ya kuku kuchakura, asili ya kinyonga kwenda kwa tahadhari, n.k.

Sifa

  1. Wahusika ni wanyama na binadamu
  2. Ni kazi ya kubuni.
  3. Hueleza kuhusu asili ya sifa, tabia au hali.
  4. Hutumia mbinu ya uhuishi.
  5. Huwa na maadili.

Umuhimu

  1. Kueleza sababu ya tabia, hali au sifa Fulani.
  2. Kuonya dhidi ya tabia hasi kama vile ulafi.
    1. Ngano za mazimwi
  • Hadithi ambazo wahusika ni mazimwi.

Sifa

  1. Wahusika ni mazimwi
  2. Mazimwi huwakilisha sifa hasi za binadamu k.m ulafi, ukatili, uovu n.k.
  3. Hujaa uharibifu.
  4. Huwa na matumizi mengi ya fantasia.
  5. Kipengele cha safari hujitokeza k.v. kwenda nchi za mbali kutafuta suluhisho.
  6. Ushindi hujitokeza (mazimwi hushindwa).
  7. Ni kazi ya kubuni.
  8. Huwa na maadili.
  9. Mazimwi huwa na sifa zinazokiuka mipaka ya binadamu k.m. kinywa kisogoni, jicho moja kubwa, n.k.

Umuhimu

  1. Kukashifu tabia ya uovu, ulafi, na ukatili.
  2. Kutahadharisha dhidi ya kuwa na ulafi, ukatili n.k.
  3. Kutia moyo waliodhulumiwa kuwa waliowanyanyasa wataadhibiwa siku moja.
    1. Ngano za Mashujaa
  • Ambazo zinazohusu watu waliotenda matendo ya kishujaa katika jamii zao kama vile kuokoa jamii.

Sifa

  1. Kipengele cha motifu au kusafiri nchi za mbali, kupigana na mazimwi kuokoa jamii.
  2. Husawiri mapigano kati ya wema (lila) na ubaya (fira).
  3. Uovu huwakilishwa na mazimwi au viongozi dhalimu
  4. Hatimaye wema hushinda uovu kwa juhudi za mashujaa
    • Ngano za mashujaa ni za kubuni ilhali katika mighani, mashujaa wanaaminiwa waliishi.

Umuhimu

  1. Kuhimiza uzalendo na ujasiri miongoni mwa vijana.
  2. Kuhimiza ujasiri miongoni mwa vijana.
  3. Kusifu mashujaa katika jamii
  4. Kuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na changamoto, inda na ila.
  5. Kuhimiza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamii.
  6. Kuonya dhidi ya matendo hasi k.v. ukatili.
  7. Kuhimiza watu kutokata tamaa
    • Ngano za mtanziko
  • Hadithi ambapo mhusika hukabiliwa hali ngumu ya kuamua baina ya mambo wawili au zaidi yanayomkabili.

Sifa

  1. Wahusika ni wanyama au binadamu.
  2. Ni kazi ya kubuni.
  3. Mhusika hulazimika kufanya uteuzi mgumu.
  4. Hali mbili au zaidi zinazotatanisha huwepo.

Umuhimu

  1. Hutuerevusha jinsi ya kupambana na hali ngumu.
  2. Kuonya/kutahadharisha dhidi ya kujiponza.
  3. Kukuza uwezo wa kupima mambo na kuteua lililo muhimu.
  4. Kuonya dhidi ya kutenda bila kuwaza kwa kina.

viii)   Ngano za Kimafumbo

  • Ambazo huwa na maana ya ndani/iliyofichika.
    1. Istiara
  • Hadithi ambayo maana yake huwakilisha maana nyingine iliyofichika k.v. hurafa ambapo wanyama huwakilisha binadamu.
  1. Mbazi
  • Hadithi fupi inayotolewa inayotolewa kama mfano kumkanya au kumwelekeza mtu k.v. katika biblia.
    1. Hadithi za Kisalua/Kihistoria
  1. Mighani
  • Hadithi za mashujaa/majagina wa jamii fulani k.m. Rwanda Magere wa Waluo, Fumo Liyongo wa Wapate, Koome Njue wa Wameru, Wangu wa Makeri wa Wakikuyu na Syokimau wa Wsakamba.

Sifa

  1. Huhusu mashujaa wa jamii fulani.
  2. Wahusika hupambana na hali ngumu inayosababishwa na maadui.
  3. Wahusika hupewa sifa na uwezo usiokuwa wa kawaida k.v. ukubwa wa ajabu, nguvu katika kivuli, nguvu katika nywele, kutoulika n.k.
  4. Wahusika hupigania haki za wanyonge.
  5. Mhusika hukomboa jamii yake dhidi ya maadui.
  6. Mhusika hufa kifo cha huzuni (tanzia) kwa kusalitiwa na mtu wa karibu k.v. mwanamke au jamaa zao.
  7. Mashujaa huuliwa kwa njia ya ajabu kama vile kunyolewa nywele, kivuli kuchomwa mkuki, kuchomwa shindano ya shaba kitovuni
  8. Mighani huzungumzia matukio ya kihistoria.
  9. Kuna tabia ya kupiga chuku matukio yaliyo hadithini.
  10. Mighani hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
  11. Huchukuliwa na jamii kama hadithi zenye ukweli na jamii hujinasibisha na mighani hiyo.
  1. Husimulia mambo ya kiimani na kidini.

Umuhimu

  1. Kutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya mighani.
  2. Kuhifadhi na kumbusha historia yajamii.
  3. Kusifu mashujaa katika jamii.
  4. Kuhimiza ujasiri miongoni mwa vijana.
  5. Kuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na adui au changamoto.
  6. Kukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamii.
  7. Kuonya dhidi ya matendo hasi kama vile usaliti.
  8. Kuhimiza watu kutokata tama.

Tofauti Kati ya Mighani na Visasili

mighani visasili
Þ    Husimulia kuhusu mashujaa.

Þ    Husimulia historia ya jamii.

Þ    Wahusika wakuu ni majagina.

 

Þ    Hueleza sifa za majagina.

Þ    Husimulia asili ya vitu.

 

Þ    Husimulia mianzo ya vitu au mambo.

Þ    Wahusika ni k.v. binadamu, miungu, wanyama, n.k.

Þ    Hueleza mianzo ya desturi.

 

  1. Visakale
    • Masimulizi ya matukio yaliyotendeka zamani k.v. vita, majanga kama njaa na magonjwa na hamahama za jamii k.v. waisraeli kutoka misri.
  • Visaviini
    • Hadithi zinazoeleza chimbuko la jamii Fulani
  1. Mapisi
    • Maelezo ya kihistoria yasiyo na ubunifu wowote k.v. chimbuko la kundi la wabantu kutoka Afrika ya Kati na kuenea sehemu mbalimbali za Afrika.
  2. Tarihi
    • Maelezo kuhusu matukio ya kihistoria kulingana na yalivyofuatana ki wakati
  3. Kumbukumbu
    • Maelezo ya kitawasifu kuhusu mtu au jamii inayotambulika kwa kutoa mchango fulani mkubwa.
      1. Vipera Vingine vya Hadithi
  1. Soga
  • Hadithi fupi za kuchekesha zinazolenga kutania au kudhihaki.

Sifa

  1. Wahusika ni wa kubuni.
  2. Hutaja ukweli unaoumiza.
  3. Hutumia vichekesho kupunguza ukali wa dhihaka.
  4. Hutumia chuku kupita kiasi.
  5. Huhusu tukio moja.
  6. Ni fupi.

Umuhimu

  1. Kukashifu matendo hasi kwa njia ya ucheshi
  2. Kuonya na kutahadharisha dhidi ya matendo hasi k.v. ulaghai.
  3. Kufunza maadili.
  4. Kuburudisha kwa kuchekesha.
    1. Vigano
  • Hadithi fupi zinazosimulia kuhusu matendo mabaya katika jamii na wakati uo huo kuonya na kuelekeza dhidi yayo.
  • Aghalabu huandamana na methali kwa lengo la kufafanua linalokusudiwa au kudhibitisha funzo la methali fulani.

Sifa

  1. Huwa vifupi.
  2. Husimulia kisa kimoja tu.
  3. Wahusika ni binadamu na wanyama.
  4. Hufunza maadili kutokana na methali.
    • Kisa
  • Masimulizi mafupi yenye tukio moja lenye funzo kwa njia ya kufurahisha.

Mambo ya Kuzingatia katika Uchambuzi wa Hadithi/Ngano

  1. Kueleza aina ya ngano kwa kuzingatia wahusika na maudhui
    • Ngano yaweza kuwa ya mazimwi na ya mashujaa kwa wakati mmoja.
    • Ngano yaweza kuwa hurafa, ya usuli na ya kiayari.
  2. Kutaja wahusika
  3. Kufafanua sifa za wahusika wakuu
  4. Maadili/mafunzo yanayojitokeza katika hadithi
  5. Kubainisha sifa za ngano/hurafa/hekaya, n.k. zinazojitokeza katika hadithi.
  6. Kueleza umuhimu wa fomyula ya kuanzia/wimbo uliotumiwa katika hadithi.
  7. Kubainisha tamathali za usemi zilizotumiwa katika hadithi fulani
  8. Kuonyesha jinsi ngano inavyoshughulikia maudhui fulani.
  9. Kufafanua ufaafu wa methali fulani zilizotumiwa katika hadithi.
  10. Katika ngano ya mtanziko, ungekuwa mhusika mkuu ungefanya nini?
  11. Kubainisha matumizi ya mbinu ya fantasia
  12. Kufafanua maswala ibuka/maudhui yaliyoshughulikiwa k.m. usaliti, ujinga, ulaghai, n.k.
  13. Kuchanganua utungo kifani-ploti, wahusika, mbinu za lugha, fantasia, nyimbo, n.k.
  14. Kueleza majukumu ya hadithi.

SEMI

  • Tungo fupi zinazowasilisha ujumbe kwa kufumba au kuchora picha.

Sifa

  1. Huwa fupi kwa kuwasilisha ujumbe mrefu kwa maneno machache.
  2. Ni tanzu tegemezi kwa hutegemea tanzu nyingine kama vile hadithi, mazungumzo, n.k.
  3. Hazibadiliki vivi hivi.
  4. Baadhi ni kielelezo cha maadili k.v. methali.
  5. Hutumia lugha ya kimafumbo.
  6. Huibua taswira.
  7. Huwa na mchezo wa maneno.
  8. Baadhi huwa na muundo maalum k.v. methali na vitendawili.
  9. Nyingine ikikosa kutumika hutoweka k.v. misimu.

Umuhimu

  1. Kuonya k.m methali, ‘Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.’
  2. Kukuza uwezo wa kufikiri k.m. vitendawili na chemsha bongo.
  3. Kutafsidi lugha au kupunguza ukali wa maneno k.m. nahau ‘jifungua’ badala ya ‘zaa’.
  4. Kuburudisha k.m. vitendawili, chemsha bongo na vitanza ndimi.
  5. Kuhifadhi siri k.m. nahau, misemo, misimu.
  6. Kuelimisha k.m. kutofanya mambo kwa pupa-mla kwa pupa hadiriki kula tamu.
  7. Kuongeza utamu katika lugha.
  8. Kuboresha matamshi k.m. vitanza ndimi.
  9. Kukuza lugha k.m misimu.
  10. Kukuza utangamano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati zinawasilishwa.

Vipera vya Semi

  1. Methali
  • Semi fupi ambazo hueleza kwa muhtasari au mafumbo ukweli fulani wa kimaisha.

Sifa

  1. Huwa fupi k.m. ‘Msafiri kafiri.’
  2. Hutumia tamathali za usemi.
  3. Hutumkia lugha ya kimafumbo.
  4. Huwa na maana ya ndani na nje.
  5. Kunazo hufanana kimaana k.m. ‘Haraka haraka haina baraka’ na ‘Polepole ndio mwendo.’
  6. Hupingana zenyewe k.m ‘Polepole ndio mwendo’ na ‘Chelewa chelewa utamkuta mwana si wako.’
  7. Huwa na sifa za kishairi k.v. ukwapi, utao na vina -Haba na haba, hujaza kiba
  8. Sifa za utegemezi kwa kuingiliana na tanzu nyingine za fasihi.
  9. Huwa na muundo maalum wa sehemu mbili:
  1. m ‘Haba na haba…’
  2. Kukamilisha wazo ‘…hujaza kibaba.’

Umuhimu

  1. Kukuza uwezo wa kufikiri kwani mpokezi hufikiri ili kupata maana ya ndani.
  2. Kuonya dhidi ya matendo yasiyofaa k.m. ‘Mchimba kisima huingia mwenyewe’na ‘Ukiambiwa jiambie usijeishia kumbe.’
  3. Kufariji walio katika hali ngumu, Baada ya dhiki faraja, Hakuna marefu yasiyo na ncha, Liandikwalo ndilo liwalo, Ajaliwalo ndilo apatalo.
  4. Kuhimiza watu kujitahidi maishani/kuonyesha jambo jema huja kwa kufanyiwa kazi k.m. ‘Mtaka cha mvunguni sharti ainame,’ ‘Chumia juani ulie kivulini.’
  5. Kupamba lugha iwe na mvuto kwani huwa na usanii mkubwa.
  6. Kuhimiza ushirikiano, ‘Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, ‘Jifya moja haliijiki chungu.’
  7. Kuelimisha mtu ajue jambo muhimu k.m. ‘Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi’, ‘Pema usijapo pema ukipema si pema tena.’
  8. Kushauri k.m. ‘Enga kabla ya kujenga’ na ‘Mchama ago hanyeli.’
  9. Kufupisha maadili katika ngano.
  10. Kubuni lakabu k.m. ‘kikulacho.’
  11. Kufunza maadili k.m. kuwa na subira-‘Subira huvuta heri.’
  12. Kuhimiza kutokata tama k.m. ‘Bandu bandu huisha gogo’ ‘Papo kwa papo kamba hukata njiwe.’
  13. Kuonyesha umuhimu wa kuthamini jamaa zako kuliko marafiki k.m. ‘Damu ni nzito kuliko maji’ ‘Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.’
  14. Kuonyesha umuhimu wa kuthamini vitu vyako-‘Usiache mbachao kwa msala upitao’ ‘Afadhali dooteni kama ambari kutanda,’
  15. Kukashifu ubinafsi k.m. ‘Mwamba ngoma huvutia kwake’ ‘Kila mchukuzi husifu mzigo wake.’
  16. Kukashifu kiburi k.m. ‘Maskini akipata matako hulia mbwata’ ‘Zingwi zingwi lipe nguo utaona mashauo.’

Mbinu za Lugha/Fani /Tamathali za Usemi katika Fasihi

  • Maneno au vifungu vya maneno vinavyotumiwa kutia fasihi urembo ili kufanya ujumbe ueleweke vyema zaidi.

Aina

  1. Tashbihi
  • Ulinganishi kwa kutumia viunganishi kama, mithili, mfano na sawa.
  1. Sitiari/ Istiara
  • Ulinganishi usio wa moja kwa moja.
  1. Tashhisi/Uhaishaji
  • Kukipa kitu sifa ya uhai.
  1. Taashira/ Ishara
  • Kitu kuwakilisha kingine.
  1. Chuku/udamisi
  • Kutia chumvi au kufanya kitu kionekane kikubwa sana au kidogo sana.
  1. Takriri
  • Urudiaji wa neno au mafungu ya maneno.
  1. Tanakuzi
  • Maneno yaliyo kinyume
  1. Tabaini
  • Msisitizo kwa njia ya kinyume kwa kutumia kikanushio si.
  1. Ritifaa
  • Kusemesha asiyekuwapo kama yupo.
  1. Taharuki
  • Kuacha msomaji akiwa na hamu ya kutaka kujua kipi kitakachojiri halafu.
  1. Majazi
  • Majina yanayooana na sifa za wahusika, vitu au mahali.
  1. Mbinu rejeshi
  • Kukumbusha mambo yaliyopita.
  1. Methali
  • Semi fupi ambazo hueleza kwa muhtasari au mafumbo ukweli fulani wa kimaisha.
  1. Nahau
  • Fungu la maneno lenye maana tofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo.
  1. Misemo
  • Semi zinazobeba ukweli wa kujumla Mifano:
  1. Mdokezo
  • Mambo kuachwa bila kumalizwa.
  1. Balagha
  • Maswali yasiyohitaji majibu.
  1. Taswira
  • Ujenzi wa picha akilini.
  1. Kinaya
  • Mhusika kutumia maneno au matendo yaliyo kinyume cha inavyotarajiwa.
  1. Koja
  • Kuorodhesha maneno na vitenzi kwa kutumia koma.
  1. Kejeli
  • Kudharau au kubeza.
  1. Jazanda
  • Kufananisha vitu kwa mafumbo k.m. katika biblia.
  1. Nidaha/ Siyahi
  • Maneno ya kuonyesha hisia za moyoni.
  1. Tanakali/onomatopeya
  • Miigo ya sauti zinazotokea baada ya kitendo.
  1. Uzungumzi nafsia
  • Kujisemesha mwenyewe.
  1. Dayalojia
  2. Utohozi/ Uswahilishaji
  3. Kuchanganya ndimi
  • Kutumia lugha ngeni.
  1. Tafsida/usafidi
  • Kutumia lugha ya adabu au kupunguza ukali wa maneno.
  1. Mkengeuko
  • Kwenda kinyume na matakwa ya jamii k.v. usenge, ndoa ya watu wasio wa rika rika moja, mapenzi nje ya ndoa.
  1. ulinganuzi
  • Kuweka pamoja mambo yanayopingana ili kulinganisha
  1. Kweli kinzani
  • Hoja mbili zinazopingana/kutowezekana.

Matumizi ya Lugha Katika Methali

Sitiari

  1. Mgeni ni kuku mweupe.
  2. Ahadi ni deni.
  3. Upweke ni uvundo.
  4. Mgeni ni kuku mweupe.
  5. Ujana ni moshi.
  6. Mapenzi ni kikohozi.
  7. Kukopa arusi kulipa matanga.

Tashbihi

  1. Kawaida ni kama sheria.
  2. Riziki kama ajali ijapo huitambui.
  3. Usilolijua ni kama usiku wa giza.
  4. Ufalme kama mvua hupiga na kupita.

Tashhisi

  1. Siri ya mtungi muulize kata.
  2. Paka akiondoka panya hutawala.
  3. Jembe halimtupi mkulima.
  4. Ukupigao ndio ukufunzao.
  5. Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.

Takriri

  1. Haba na haba hujaza kibaba.
  2. Chovya chovya humaliza buyu la asali.
  3. Hauchi hauchi unakucha.
  4. Hayawi hayawi huwa.
  5. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
  6. Bandu bandu huisha gogo.

Balagha

  1. Pilipili usiyoila yakuwashiani?
  2. Angurumapo samba mcheza ni nani?
  3. Wameshindwa wenye pembe seuze wewe kipara?
  4. Simba mla watu akiliwa huwani?
  5. Mzigo uko kichwani, kwapa lakutokeani jasho?
  6. Mavi usiyoyala wayawingiani kuku?
  7. Mla ni mla leo mla jana kalani?

Taswira

  1. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
  2. Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
  3. Mtupa jongoo hutupa na ung`ong`o wake.
  4. Angeenda juu kipungu hafikii mbingu.

Chuku

  1. Mzigo wa mwenzio ni kanda la sufi.
  2. Maji ya kifuu bahari ya chungu.
  3. Usipoziba ufa utajenga ukuta.

Tanakali za sauti

  1. Chururu si ndondondo!
  2. Ndo! Ndo! Hujaza ndoo.
  3. Kiliacho pa kijutie.

Kinaya

  1. Bara Hindi ndiko kwenye nguo na waendao uchi wapo.
  2. Kwenye miti hakuna wajenzi.
  3. Asante ya punda ni mateke.
  4. Kigumba kwa nguruwe kwa binadamu ki uchungu.
  5. Kikiharibika cha fundi kikiongoka cha bwana Sudi.

Kejeli/dhihaka/stihizai

  1. Umekuwa mung`unye waharibikia ukubwani.
  2. Hawi Musa kwa kubeba fimbo.
  3. Ucha Mungu si kilemba cheupe.
  4. Kichwa cha kuku hakistahili kilemba.
  5. Kichwa cha nyoka hakibandikwi mtungi.

Jazanda

  1. Joka la mdimu hulinda watundao
  • Mtu mwovu huwanyima wengine vitu asivyovihitaji.
    1. Kupanda mchongoma kushuka ndio ngoma
  • Ni rahisi kujitia katika matata kuliko kujitoa.

Taashira

  1. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.
  2. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.

Kweli kinzani

  1. Wagombanao ndio wapatanao.
  2. Ukupigao ndio ukufunzao.
  3. Kuinamako ndiko kuinukako.
  4. Mwenye kelele hana neno.
  5. Kimya kingi kina mshindo mkubwa.

Tanakuzi

  1. Tamaa mbele mauti nyuma.
  2. Mpanda ngazi hushuka.
  3. Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi.
  • Kuainisha methali kutokana na matumizi ya lugha ni kusema mbinu ambazo imetumia.

Vigezo vya Kuainishia Methali/Kuziweka Pamoja na kuzichambua

  1. Mandhari/mazingira k.m. kilimo.
  • Ukipanda pantosha utavuna pankwisha.
  • Jembe halimtupi mkulima.
    1. Maudhui k.m. ulezi
  • Samaki mkunje angali mbichi.
  • Mcha mwana kulia hulia yeye
  1. c) fani/tamathali k.m. takriri
  • Haba na haba hujaza kibaba
  • Mtoto wa nyoka ni nyoka.
  1. d) Jukumu k.m. kuonye
  • Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  • Ukiambiwa jiambie usijeishia kumbe.
    1. Maana k.m. sawa
      • Haraka haraka haina baraka.
      • Polepole ndio mwendo.

Vigezo zaidi vya kuchambua methali

  1. Inarejelea vitu gani? K.m. Hindi ndiko kwenye nguo na waendao uchi wapo.
  • Nchi-Hindi
  • Vitu-nguo
  • Watu-waendao uchi
    1. Inakupa wazo gani kuhusu jamii husika?
  • Utamaduni na njia za kiuchumi.
    1. Vitendawili
  • Semi ambazo hutolewa kwa mtu kwa mfano wa swali ili azifumbue.

Sifa

  1. Huwa vifupi kimaelezo.
  2. Hutumia lugha ya kimafumbo.
  3. Hutolewa mbele ya hadhira.
  4. Hutumia ufananisho wa kijazanda.
  5. Kunazo huhusiana na methali k.m. mzee amekufa vyombo vimevunjikavunjika.
  6. Huwa na wakati maalum wa kutolewa yaani jioni.
  7. Huwa na mchezo wa maneno k.m. Ukiona njigi utadhani njege.
  • Maziwa na tui
  1. Hujisimamia vyenyewe.
  2. Kunavyo huwa na jibu zaidi ya moja k.v. Gari la kila mtu
  • miguu, kifo au jeneza
  1. Hutumia tamathali za lugha kwa ufanifu mkubwa
  2. Huweza kuwa na fomyula/muundo maalum
    1. Mteguaji: Kitendawili
    2. Mteguaji: Tega
  • Mteguaji: Kitendawili chenyewe- Popoo mbili zavuka mto
  1. Mteguaji : Mlango
  2. Mtegaji: Umenoa. Nipe mji.
  3. Mteguaji: Ninakupa Nairobi.
  • Mteguaji: Nilienda Nairobi watu wa Nairobi wakaniambia nije niwasalimu. Jibu ni macho.

Umuhimu

  1. Kuburudisha jioni baada ya kazi.
  2. Kukuza ubunifu wa kuvitunga kwa kulinganisha vitu katika mazingira ili kuviunda.
  3. Kuimarisha uwezo wa kukumbuka.
  4. Kukuza uwezo wa kufikiri kwani mfumbiwa huhitaji kufikiri sana ili kupata jibu.
  5. Kuleta umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati vinategwa.
  6. Kuimarisha ujuzi wa kujieleza kwa lugha.
  7. Kupanua ujuzi wa mazingira wa mtoto.
  8. Kuendeleza utamaduni wa jamii k.m. Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini. siwezi kulichuma
  • Ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike.
  1. Kukejeli au kudharau tabia mbaya k.m. Wazungu wawili wanachungulia dirishani
  • makamasi

Aina za vitendawili

  1. Sahili
    • Vina muundo rahisi/maneno machache k.m Akiona mwangaza wa jua hufa-samaki.
  2. Tata
  • Vyenye majibu tofauti
    1. Kisimulizi
  • Masimulizi k.m. Kulikuwa na baba ng’ambo moja ya mto na binti zake wawili ng’ambo ya pili. Alikuwa na maembe mawili aliyopaswa kuyavukisha pamoja apelekee binti zake. Angefanya nini?
    1. Vya tanakali k.m. Parrrr! Mpaka Makka-utelezi.
    2. Mkufu
  • Vyenye sehemu zinazochangizana kimaana k.m. Nikitembea yuko lakini nikiingia nyumbani hupotea-kivuli.

Matumizi ya Lugha Katika Vitendawili

Tashhisi

  1. Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi-giza.
  2. Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi hupendeza mno-ndizi.
  3. Anakula lakini hashibi-kifo/mauti.
  4. Amchukuapo hamrudishi-kaburi.
  5. Akizungumza kila mtu hubabaika-radi.
  6. Daima nasababisha mafarakano-uke wenza.
    • Tashbihi
  7. Boi wangu kazama kaibuka kama mzungu-mwiko wa ugali.

Sitiari

  1. Bibi hatui mzigo-konokono.
  2. Mamangu hachoki kunibeba-kitanda.
  3. Fatuma mchafu-ufagio.
  4. Saa yetu kadiri inavyotembea ndivyo inavyopunguza nguvu-moyo.
  5. Mzungu kujishika kiuno- kikombe.
  6. Nina mapapai yangu mawili ambayo siwezi kuyala- matiti ya mwanamke.
  7. Ng`ombe wangu nisipomshika mkia hali nyasi-jembe.
  8. Kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi-jina.
  9. Popoo mbili zavuka mto-macho.
  10. Gari la kila mtu-miguu.
  11. Dada ni mrembo lakini akiguzwa analia-papai.

Takriri

  1. Huku ng`o na kule ng`o-giza.
  2. Amezaliwa Ali, amekufa Ali, amerudi Ali-nywele.
  3. Huku fungu katikati bahari-naz.i

Tanakali

  1. Parrr! Mpaka Makka-utelezi.
  2. Huku pi kule pi-mkia wa kondoo atembeapo.
  3. Ba funika ba funua (Bak bandika, bak bandua)-nyayo.
  4. Tang! Yaanguka-sarafu.

Kweli kinzani

  1. Ana meno lakini hayaumi-kitana.
  2. Ajenga ingawa hana mikono-ndege.
  3. Hukopa lakini halipi-kifo.
  4. Nina shamba langu kubwa lakini nikivuna halijai hata kofi-nywele.
  5. Hufa akifufuka-bahari kupwa.
  6. Nameza lakini sishibi-mate.

Taswira

  1. Adui tumemzingira lakini hatumwezi-moto.
  2. Nyama nje, ngozi ndani, mchanga ndani-firgisi ya kuku.
  3. Wanatazamana tu lakini hawaamkiani-ardhi na bingu.
  4. Askari wangu wote wamevaa kofia upande-mahindi shambani.
  5. Samaki wangu aelea kimgongomgongo-merikebu.
  6. Babu amebeba machicha meupe kichwani- mvi.

Stihizai/dhihaka/kejeli

  1. Akivaa miwani hafanyi kazi vizuri-mlevi.
  2. Mzungu anachungulia dirishani-makamasi.
  3. Uzi mwembamba umefunga dume-usingizi.
  4. Mtani wangu hata akiishi majini hatakati-chura.
  5. Kisiki chetu hakikui-mbilikimo.
  6. Nimemuona bi kizee amejitwika machicha-mvi.

Jazanda

  1. Mungu alinipa shilingi mbili, moja nitumie nyingine niweke-ardhi na mbingu.
  • Kuchambua kitendawili kwa kueleza mbinu za lugha zilizokiunda.

Kulinganisha vitendawili na methali

Kufanana

  • Zote mbili ni tungo fupi.
  • Zote mbili huwa na maana fiche.
  • Zote mbili hutumia lugha inayojenga taswira.
  • Zote mbili hupata maana kulingana na jamii.
  • Zote mbili Huwa na muundo maalum.
  • Zote mbili hufumbata ukweli fulani wa kijamii.

Tofauti

Vitendawili Methali
ü  Vina fomyula maalum ya uwasilishaji.

ü  Fumbo lazima lifumbuliwe papo hapo.

ü  Maarufu zaidi miongoni mwa watoto/vijana.

 

 

ü  Hutolewa katika vikao maalum.

ü  Hadhira tendi inayotoa maana

ü  Hutumia lugha ya majibizano.

ü  Hazina fomyula.

 

 

ü  Fumbo halifumbuliwi papo hapo.

ü  Kuonyesha hekima hasa miongoni mwa watu wazima na wazee.

ü  Si lazima zitengewe vikao.

ü  Hadhira si tendi.

 

ü  Kauli moja ya msemaji

  • Chemsha Bongo
  • Maswali ambayo huhitaji mtu kutumia akili na ujuzi kuyajibu.
  • Mafumbo ni kauli zenye maana iliyofichika na hujumuisha vitendawili na chemshabongo.

Mifano

  1. Kilo moja ya chuma na kilo moja ya nyama ipi nzito?
  2. Amada ana wafanyikazi saba, wanne hufanya kazi vizuri, wawili ni kama wamekufa, mmoja ni kama mwenda wazimu- miguu, pembe na mkia wa ng’ombe.
  3. Kipungu alipita juu, mama na ndege wawili wakamwangalia. Je macho mangapi yalimuona kipungu?- manne.
  4. Nina watu wangu watatu, wawili ni watoto na wawili ni baba- mtoto, baba na babu.
  5. Chura alitumbukia katika shimo la futi 30 na anaruka futi 10. Aruke mara ngapi ili atoke?- Hawezi.
  6. Watu watatu wanavuka mto. Mmoja aliyaona maji na kuyakanyaga. Wapili aliyaona lakini hakuyakanyaga. Watatu hakuyaona wala kuyakanyaga. Watu hao ni kina nani?

Sifa

  1. Ni kauli fupi au ndefu.
  2. Hutuia lugha ya kimafumbo.
  3. Hutumia ufananisho wa kijazanda.
  4. Huhitaji mtu kuwaza ili kupata jibu.
  5. Hujengwa na vitu vinavyotokana na mazingira.
  6. Hazina muundo maalum kama methali, nahau na vitendawili
  7. Hupima uwezo wa msikilizaji wa kutambua jambo lililofichwa.

Umuhimu

  1. Kuimarisha stadi ya kusikiliza.
  2. Kunoa uwezo wa kufahamu.
  3. Kutoa mawaidha.
  4. Kufunza kuhusu maumbile.
  5. Kuimarisha uwezo wa kukumbuka.
  6. Kufunza mambo kuhusu mazingira na maumbile.
  7. Kukuza uwezo wa kutumia lugha.
  8. Kukuza uwezo wa kufikiri.
  9. Kuburudisha na kuchekesha.
  10. Kukuza uwezo wa kubuni.
    • Vitanza Ndimi
  • Sentensi zenye mfuatano wa sauti zinazotatanisha kimatamshi zinapotamkwa kwa haraka.

Mifano

  1. Wataita wataita Wataita wa Taita.
  2. Waite wale wana wa liwali wale wali wa liwalii
  3. Kupa mpe akupao kumpa asokupa si kupa ni kutupa.
  4. Shirika la Reli la Rwanda limefungwa.
  5. Hilo lililoliwa ndilo nililolitaka.
  6. Mchuuzi wa mchuzi hana ujuzi wa mjusi wa juzi.
  7. Cha mkufuu mwanafuu ha akila hu cha mwanafuu mkufuu hu akila ha
  8. Pema usijapo pema ukipema si pema tena
  9. Nguo zisizotakikana zitachomwa zote.

Sifa

  1. Ni kauli fupi.
  2. Huwa na mchezo wa maneno.
  3. Huundwa kwa sauti zinazokaribiana kimatamshi.
  4. Hutumia maneno yenye maana zaidi ya moja au yenye sauti sawa.
  5. Hutanza/hutatiza ndimi za wengi wakalemewa kutamka.
  6. Hukanganya kimatamshi.

Umuhimu

  1. Kukuza matamshi bora mtu anapoendelea kutamka.
  2. Kukuza uwezo wa kufikiri haraka ili kujua maana za maneno ili kutamka ipasavyo.
  3. Kupanua ujuzi wa msamiati.
  4. Kuburudisha kwa kufurahisha na kuchangamsha.
  5. Husaidia kutofautisha maana za maneno.
  6. Kujenga stadi ya kusikiliza.
  7. Kukuza ubunifu kwa kuteua maneno yanayotatanisha kisauti na kimaana.
  8. Kujenga uhusiano bora kwa ucheshi.
    1. Lakabu
  • Jina la msimbo/kupanga/ambalo mtu hupewa au hujipa kutokana na sifa zake.

Asili ya Lakabu

  1. Tabia
  2. Sifa za kimaumbile
  3. Matendo
  4. Nasaba atokayo mtu.
  5. Tabaka
  6. Jinsi mtu anavyotamka maneno k.m. ung’eng’e.

Mifano

  1. Nyayo
    • Moi
  2. Simba wa Yuda
  • Haille Selassie
  1. Mkuki uwakao
  • Kenyatta
  1. Nyundo/Tingatinga
  • Raila
  1. Baba wa taifa
  • Rais
  1. Mama wa Taifa
  • Mke wa Rais

Sifa

  1. Huwa neno au fungu la maneno kadha.
  2. Huwa na maana iliyofumbwa.
  3. Huoana na sifa hasi au chanya za aliyepewa.
  4. Huwa za kusifu au kudhihaki.
  5. Huweza kudumu hata kusahaulisha jina halisi la mtu.
  6. Hutumia sitiari k.m. chui kumaanisha mkali.
  7. Hutumia taswira.
  8. Hushika sana kimatumizi miongoni mwa watu.

Umuhimu

  1. Kufahamisha sifa za mtu kwa kifupi.
  2. Huwa njia ya washairi ya kujitangaza bila kujisifu moja kwa moja.
  3. Hutumiwa kama ishara ya heshima kwa anayestahili heshima k.m. kiongozi.
  4. Kuficha utambulisho au jina halisi la mtu.
  5. Hutumiwa katika majigambo na mhusika kuonyesha ubingwa wake.
  6. Kuficha siri ili anayemrejelewa asijulikane k.m. kikulacho.
  7. Kukuza uhusiano bora miongoni mwa watani wanaporejeleana kwa lakabu.
  8. Kusifu tabia njema kwa kumpa mtu lakabu nzuri.
  9. Kudhihaki au kukashifu tabia mbaya kwa kumpa mtu lakabu mbaya
  10. Kutambulisha asili ya mtu.
    • Misemo
  • Semi zinazobeba ukweli wa kijumla.

Mifano

  1. Binadamu ni udongo.
  2. Mwili haujengwi kwa mbao.
  3. Umaskini si kilema.
  4. Lila na fira havitangamani.
  5. Ndio kwanza mkoko ualike maua.
    • Mambo kuzidi kushika kasi.
  6. Mgomba haupandwi changaraweni ukamea
  • Jambo halifanywi mahali pasipofaa likapendeza.

Sifa

  1. Hutumia lugha ya muhtasari.
  2. Hutoa ukweli kwa jumla.
  3. Hazina muundo maalum.

Umuhimu

  1. Kusisitiza ujumbe.
  2. Kuongeza utamu katika lugha.
  3. Kusisitiza jambo fulani.
  4. Kufunza maadili au kuhimiza.
  5. Kuchochea hisi fulani.
    • Nahau

Fungu la maneno lenye maana tofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo.

Mifano

 

  1. Kuasi ukapera
    • kuoa
  2. Kupiga vijembe
  • sema kwa mafumbo
  1. Ndege mbaya
  • bahati mbaya
  1. Kidudu mtu
  • mfitini
  1. Paka mafuta kwa mgongo wa chupa
  • Danganya au hadaa mtu
  1. Visha kilemba cha ukoka
  • Mpa mtu sifa za uongo ili umpumbaze
  1. Kubali shingo upande
  2. Kuyavulia maji ngu
  • kumaliza jambo fulani ulilolianzia
  1. Arusi ya ndovu kumla mwanawe
  • kubwa

 

Sifa

  1. Hutumia lugha ya kimkato.
  2. Maneno huwa na maana tofauti na ya kawaida.
  3. Kunazo huwa na maana zaidi ya moja k.v. kuja jamvi-kumaliza shughuli au kuondoka.
  4. Huundwa kwa neno moja, mawili au zaidi.
  5. Huibua taswira.
  6. Zina muundo maalum/huundwa kwa aina mbalimbali za maneno.

 

  1. T+T
  • kufa kupona
  • kufumba na kufumbua
    1. T+N
  • kupiga domo
  • kata kamba
    • T+E
  • Kujikaza kisabuni
  • kufa kiofisa
    1. N+N
  • donda dugu
  • domo kaya
    1. N+V
  • nyota njema
  • dege mbaya
  1. N+T
  • damu kumkauka
  • akili kumruka

 

Umuhimu

  1. Kukuza na kuendeleza msamiati wa maneno.
  2. Kupunguza ukali wa maneno (tafsida).
  3. Kuongeza utamu/ladha katika lugha.
  4. Kuhifadhi siri kwani sio wote wanajua maana.
  5. Kujaribu uwezo wa msikilizaji kufichua maana iliyofichika.
    • Misimu/simo
  • Semi ambazo huzuka katika mazingira na kipindi fulani.

Aina za Mizimu

  1. Inayotumika na kutoweka
  2. Inayokita kimatumizi kuingizwa katika Kiswahili sanifu k.m. toa chai, chokora, n.k.

Asili

 

  1. Ufupishaji maneno
    • komp
  2. Utohozi
  • Fathee
  • hepi
  1. Sitiari/jazanda
  • nyani-mlinda lango
  • fisi- mlafi
  1. Tanakali
  • mtutu- bunduki
  • ndala- malapulapu
  1. Uundaji maneno mapya
  • hanya
  1. Kupa maneno maana mpya
  • chuma-gari
  • toboa- faulu
  1. Kugeuza maneno
  • risto-stori
  1. Kuboronga lugha
  • ashu-ashara/kumi

Mifano

  • Jisikia sukari
    • kuringa
  1. Kaa ngumu
  • kutotishika/kuvumilia
  1. Chongoa mtu
  • mfanyia mzaha
  1. Kula njaro
  • kupuuza kazi
  1. Piga nduthe
  • kimbia/toroka
  1. Piga ngeta
  • kukaba koo
  1. Leta diambo
  • zozana/lalamika
  1. Ingia baridi
  • kuogopa
  1. Pewa msomo
  • gombezwa
  1. Kusota
  • kuishiwa na pesa
  1. Ingia mitini
  • toweka/toroka
  1. Kung`ara
  • kuvaa vizuri
  1. Marehemu George
  • nguo za mitumba
  1. Vaa chupa
  • vaa suruari nyembamba
  1. Kujisikia poa
  • kuwa na furaha
  1. Kula hepi
  • kuburudika
  1. Lala kibahasha
  • tulia tuli baada ya kushindwa katika jambo

 

Sifa

  1. Ni kauli fupi.
  2. Hutumiwa na kundi dogo la watu.
  3. Huzuka katika mazingira na kipindi maalum.
  4. Ni lugha ya kimafumbo.
  5. Hutumiwa na kundi dogo la watu katika jamii.
  6. Huzuka na kutoweka baada ya muda.
  7. Kunazo hudumu na kukubaliwa kama lugha sanifu k.v. matatu, bodaboda, chai, chokora, daladala, n.k.
  8. Huwa na maana nyingi k.m. ‘mahewa’ humaanisha mziki, uongo au ulevi wa dawa za kulevya.
  9. Maneno yana maana tofauti na ya kawaida.
  10. Si lugha sanifu na hivyo haipaswi kutumiwa katika mazungumzo rasmi.
  11. Hupendeza miongoni mwa watumizi.
  12. Hutoweka baada ya matumizi kwa muda.
  13. Hubadilika k.m. mbuyu na buda humaanisha baba.

Umuhimu

  1. Kuficha siri ya wanaoitumia.
  2. Kupanua lugha kimsamiati ikikubalika.
  3. Kurahisisha mawasiliano kwa kuondoa uchovu wa urasmi.
  4. Kuonyesha ubingwa wa lugha kwa kuhisi huonyesha umaarufu wa lugha
  5. Kutenga wasio wana kikundi.
  6. Kutafsidi/kupunguza ukali wa maneno k.m. Amepata bol-mimba.
  7. Kupamba lugha na kuifanya ivutie
  8. Kufanya wanakikundi wajihisi kuwa pamoja.
  9. Kujitambulisha na watu wa kikundi fulani.
    1. Shirikina
  • Semi ambazo huonyesha imani fulani ya kundi ya watu

Mifano

  1. Ukijikuna kiganja cha mikono utapata pesa.
  2. Ukila chakula gizani utakula na shetani.
  3. Kuzaliwa ukiwa na vidole sita ni kuwa na bahati.
  4. Bundi akilia karibu na nyumba mtu mmoja wa nyumba ile atafariki.

Umuhimu

  1. Kukataza maovu.
  2. Kuhifadhi utamaduni.
  3. Kuchangia umoja wa kitaifa kwa aina moja ya itikadi kupatikana katika jamii nyingi.
  4. Kutujulisha kuhusu itikadi za watu.
    1. Tanakali za Sauti (Onomatopeya)
  • Maneno ambayo huiga sauti ya jambo, tendo au tukio fulani

Mifano

  1. Boboka bobobo!
  • payuka ovyo ovyo
  1. Bwakia bwaku
  • akia upesi upesi
  1. Bwatika bwata
  • enda chini kwa mshindo
  1. Bweka bwebwebwe!
  • lia kama mbwa
  1. Chaga ngungundu
  • shikilia jambo
  1. Ng’o!
  • kutoambulia chochote
  1. Legalega lege
  • kosa kuwa imara
  1. Chakua nyakunyaku
  • tafuna kwa kutoa sauti ya kuudhi
  1. Bingirika bingiribingiri!
  • pinduka
  1. Birua biru!
  • angusha na kupindua
  1. Shindilia ndi!

       Mianguko

  1. Pu/kacha
  • tawi
  1. Pu, pu, pu
  • mfululizo
  1. Pukupuku!
  • mvua
  1. Pwa!
  • kwa matope
  1. Pwata!
  • kitu kinene
  1. Tang’!
  • sarafu pagumu
  1. Tapwi
  • matopeni
  1. Tifu
  • mchangani
  1. Tubwi/ chubwi
  • majini

 

Sifa

  1. Ni kauli fupi.
  2. Ni miigo ya sauti zinazotokea baada ya tendo fulani.
  3. Hazina muundo maalum.
  4. Hujumuishwa katika fani nyingine.
  5. Hutumia takriri.

Umuhimu

  1. Kuwezesha kuunda taswira ya jinsi mambo yanavyotokea.
  2. Kuonyesha hisia fulani.
  3. Kuongeza uzito kwa maneno.
  4. Kuongeza utamu katika mazungumzo.
  5. Kusisitiza jambo.
  6. Kuipa lugha ladha na mvuto.
  7. Kujenga tabia ya kusikiliza kwa makini ili kutambua mlio.
  8. Kukuza ustadi wa kuiga na kuigiza.
  9. Ni mbinu mojawapo ya mawasiliano.
    1. Takriri za maana
  • Mafungu ya maneno yanayosisitiza na kueleza maana zaidi ya kitendo.

Mifano

  1. Haambiliki hasemezeki
  2. Siku nenda siku rudi
  3. Tilia huku ukitolea kule
  4. Hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini

Umuhimu

  1. Kutia ladha katika lugha na kuifanya iwe na mnato.
  2. Kusisitiza jambo.
  3. Kuonyesha ukwasi wa lugha ya mnenaji.
    • Tashbihi
  • Misemo ya ulinganisho

Sifa

  1. Ni fupi.
  2. Hutumia viungio kama, mithili ya, n.k.
  3. Huwa na ujumbe wa kina.
  4. Hutoa taswira ambayo husaidia keleza hulka kikamilifu.

Umuhimu

  1. Kueleza sifa za kinazozungumziwa
  2. Kuongeza lugha utamu
  3. Kuonyesha umilisi wa lugha wa mtumizi

USHAIRI

  • Utanzu wa fasihi unaotumia lugha ya mkato inayoeleza maudhui yake kwa ufupi.

Sifa

  1. Hutumia lugha ya kimkato.
  2. Huwasilishwa mbele ya hadhira.
  3. Huwasilishwa na mtu mmoja au kundi la watu.
  4. Huwa na muundo maalum k.v. beti, vipande na vina.
  5. Hutegemea sauti iliyo kipengele muhimu.
  6. Huandamana na ishara za mikono, uso n.k.
  7. Una mpangilio maalum wa maneno.
  8. Una uteuzi maalum wa maneno.
  9. Uwasilishaji wake huandamana na vitendo/uigizaji.
  10. Hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa mdomo.
  11. Huandamana na shughuli maalum k.v. matanga, kazi, n.k.
  12. Huwa na mapigo ya kimziki au huweza kuimbika.
  13. Huweza kuambatana na ala za mziki.
  14. Hadhira hushiriki katika uwasilishaji wa ushairi simulizi.

Majukumu

  1. Kuburudisha watu katika sherehe au shughuli fulani ya kijamii.
  2. Kutakasa hisia au kutoa hisia zinazomsumbua mtu.
  3. Kufunza maadili au tabia zinazokubalika na jamii.
  4. Kufariji watu kutokana na maafa, kifo au kushindwa.
  5. Kukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga waliotendea jamii mambo makuu k.v. mashujaa.
  6. Kuhifadhi historia ya jamii k.m. maghani simulizi na tenzi.
  7. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii.
  8. Kuelimisha kuhusu suala fulani.
  9. Kukashifu/kukejeli sifa mbaya za wabaya.
  10. Kukuza umoja na ushirikiano katika jamii kwa kujumuisha watu pamoja.
  11. Kusifu na kutukuza mashujaa katika jamii (tenzi).
  12. Kukanya/kutahadharisha dhidi ya matendo maovu.
  13. Kukuza urembo au usanii wa lugha kwa kuwa una ufundi mkubwa wa matumizi ya lugha.
  14. Kuhamasisha jamii k.v. kisiasa.
  15. Kukuza ubunifu kwa mtunzi na mwasilishaji
  16. Kukuza ubunifu kwa kutunga kwa kuzingatia beti, mizani, vina na uteuzi maalum wa maneno.

Vipera vya Ushairi

  1. wimbo
  2. maghani
  3. mashairi mepesi (utungo unaokaririwa)
  4. ngojera (kwa majibizano)
  5. tendi au rara (husimuliwa kwa mapigo ya kishairi)
    1. Wimbo
  • Uungo wenye mahadhi ya kupanda na kushuka

Sifa

  1. Huwasilishwa kwa njia ya mdomo.
  2. Hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti.
  3. Hutumia lugha ya mkato.
  4. Hadhira yaweza kuwepo au isiwepo.
  5. Huwa na mwimbaji au waimbaji wanaoimba.
  6. Waimbaji wanaweza kujivika maleba.
  7. Huweza kuambatana na ala k.v. ngoma, zeze, kayamba n.k.
  8. Huwa na urudiaji wa mstari au kifungu.
  9. Aghalabu huimbwa na kupokezanwa baina ya kiongozi na waimbaji
  10. Huimbwa tu au huambatana na kucheza.
  11. Huweza kuandamana na shughuli fulani k.v. arusi, kazi, matanga, n.k.
  12. Huwa na muundo maalum wa beti, mistari, vina, k.

Majukumu

  1. Kuburudisha k.m. tumbuizo.
  2. Nyenzo ya kiuchumi kwa baadhi ya watu.
  3. Kuliwaza k.m. mbolezi.
  4. Kuhimiza watu wakiwa kazini k.m. hodiya.
  5. Kuelimisha kuhusu suala fulani k.m. ukimwi, ufisadi, n.k.
  6. Kuhimiza uzalendo k.m. za siasa na taifa.
  7. Kumbembeleza mtoto aache kulia au alale k.m. bembelezi.
  8. Kukashifu/kukejeli mwenendo mbaya k.v. uchoyo, vivu, n.k.
  9. Kufunza maadili au tabia inayokubaliwa na jamii k.v. ukarimu, uaminifu, n.k.

Ubaya wa nyimbo

  1. Kutumiwa kueneza hisia za kikabila.
  2. Kutia watu kasumba.
  3. Hutumiwa kueneza propaganda ili kushawishi watu.
  4. Kupotosha kimaadili k.v. kuhimiza zinaa.
  5. Mtu akizizoea humlevya.

Aina za nyimbo

  1. Bembelezi/bembea
  • Nyimbo zilizoimbwa kumbembeleza/kumwongoa mtoto aache kulia au alale.

Sifa

  1. Huimbwa na mama au walezi.
  2. Aghalabu huwa fupi.
  3. Huimbwa kwa sauti ya chini.
  4. Huimbwa kwa sauti nyororo.
  5. Zina mapigo ya polepolena taratibu.
  6. Huwa na mahadhi mazuri.
  7. Huimbwa aghalabu mtoto akiwa amebebwa kwa mbeleko na mwimbaji akimpapasapapasa.
  8. Zina urudiaji wa maneno ya kibwagizo.
  9. Huwa na lugha ya kushawishi k.v. kutoa ahadi ya kununulia mtoto zawadi.

Majukumu

  1. Kumnyamazisha mtoto anapolia.
  2. Kuwaongoa watoto walale.
  3. Kutumbuiza watoto.
  4. Kusuta wasiowapa watoto malezi mema.
  5. Kuonya mtoto dhidi ya tabia hasi k.v. kulia ovyo.
  6. Kusifu mtoto.
  7. Kuonyesha msimamo wa jamii kuhusu mtoto.
  8. Kumfariji mtoto k.m. kutokana na kuumia akicheza.
    1. Nyimbo za watoto/chekechea
  • Zilizoimbwa na watoto wakati wa kucheza/shughuli zao

Majukumu

  1. Kuburudisha watoto.
  2. Kuwaelimisha watoto kuhusu jamii.
  3. Kukuza umoja na ushirikiano baina ya watoto kwa kuwajumuisha pamoja na kucheza bila kujali kabila, tabaka, n.k.
  4. Kukashifu tabia hasi miongoni mwa watoto k.v. uchoyo.
  5. Kukuza ubunifu miongoni mwa watoto wanapobuni nyimbo zinazooana na michezo yao.
  6. Kuifanya michezo ya watoto ipendeze.
  • Nyimbo za sifa/sifo
  • Za kujisifu au kusifu mtu kwa mchango wake katika jamii.

Sifa

  1. Zaweza kuwa nyiso, za arusi za kutawazwa n.k.
  2. Huimbwa katika muktadha maalum k.v. arusini, jandoni, n.k.
  3. Hutumia sitiari au kufananisha na mnyama, mkuki, n.k.
  4. Hupiga chuku sifa za anayesifiwa.

Majukumu

  1. Kusifu mtu kutokana na matendo yake mazuri.
  2. Kutangaza mchango na mafanikio ya anayesifiwa.
  3. Kukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga matendo mazuri ya anayesifiwa.
  4. Kuburudisha watu katika sherehe fulani.
  5. Kuangazia matendo ya wahusika.
    1. Hodiya/yimbo za Kazi
  • Zilizoimbwa wakati wa kazi.

Sifa

  1. Huimwa watu wakifanya kazi k.v. uwindaji, ukulima, uvuvi, ubaharia, n.k.
  2. Huimbwa na mfanyakazi mmoja au kundi lao.
  3. Zina maneno ya kuhimiza.
  4. Urefu wake hutegemea kazi.
  5. Mdundo hutegemea kasi ya kazi ikama inafanywa kwa kasi mdundo ni wa kasi, kama polepole mdundo ni wa polepole.

Majukumu

  1. Kuburudisha watu wakifanya kazi.
  2. Kurahisisha kazi kwa kupunguza fikra za uchovu.
  3. Kuhimiza bidii kazini.
  4. Kuhimiza watu wapende kazi zao.
  5. Kuondoa uchovu na ukinaifu wakati wa kazi.
  6. Kuwatia moyo wafanyakazi wasikate tamaa.
  7. Kutambulisha jamii kwa kuonyesha shughuli zake za kazi.
  8. Kusifu kazi.
  9. Kukashifu uvivu.
  10. Kuonyesha matatizo na changamoto za wafanyikazi.
  11. Kujenga umoja na ushirikiano baina ya wafanyakazi wanapoziimba pamoja. Aina za hodiya
    1. Wawe/vave
  • Zinazoimbwa wakati wa kulima.
    1. Nyimbo za uwindaji
  • Zilizoimbwa watu wakienda au kutoka katika uwindaji.

Majukumu

  1. Kumburudisha mwindaji.
  2. Kumtoa mwindaji upweke.
  3. Kusifu mnyama.
  4. Kujasirisha wawindaji.
  5. Kimai
    • Zinazoimbwa katika shughuli za majini k.v. uvuvi na ubaharia.

Majukumu

  1. Kuburudisha wavuvi na mabaharia.
  2. Kuwajasirisha ili kukabili adha za baharini.
  3. Kuwatoa upweke.
    1. Nyimbo za mapenzi
      • Zilizoimbwa kutoa hisia za mapenzi.

Sifa

  1. Huwa na ujumbe wa kimapenzi.
  2. Maneno matamu yenye hisia nzito.
  3. Matumizi ya chuku k.m. sili wala silali.
  4. Huwa zina sifa au kashfa.

Mjukumu

  1. Kuburudisha anayezisikiliza.
  2. Kuomba uchumba au mapenzi.
  3. Kusifu tabia au urembo/umbo la mpenzi.
  4. Kusifu wapenzi.
  5. Kukashifu mpenzi asiye na sifa nzuri.
  6. Kusuta waliodhani penzi lisingefaulu.
  7. Kupunguza uzito wa hisia k.v. huzuni au udhia baada ya kusalitiwa na mpenzi.
  1. Nyimbo za arusi
    • Zinazoimbwa wakati wa kufunga ndoa.

Sifa

  1. Huimbwa kuonyesha hisia za wazazi, jamaa na marafiki
  2. Hushauri maharusi na waliohudhuria kuhusu majukumu ya ndoa
  3. Wakati mwingine husifia maharusi.

Majukumu

  1. Kutumbuiza maharusu na waliohudhuria.
  2. Kusifu maharusi.
  3. Kutoa pongezi kwa Bw. na Bi. arusi kwa kujihifadhi vyema.
  4. Kufunza majukumu ya ndoa.
  5. Kutoa mwongozo wa kupambana na vikwazo ndoani
  6. Kusuta mahasidi waliodhani ndoa isingefaulu.
  7. Kukanya na kutahadharisha watu wanaoingilia ndoa za watu kuziharibu.
    • Nyimbo za Dini
      • Zilizoandamana na shughuli za kidini.

Majukumu

  1. Kuabudu Mungu ama miungu.
  2. Kusifu mungu/miungu.
  3. Kutoa shukrani kwa mungu.
  4. Kuomba mema kutoka kwa Mungu au miungu.
  5. Kutoa mafunzo ya kidini.
  • Tumbuizo
    • Nyimbo za kujipa burudani
    • Huimbwa wakati wa mapumziko

Majukumu

  1. Kutumbuiza watu k.v. ngomani, arusini, n.k.
  2. Kuwapa vijana mwongozo/kuadilisha.
  1. Nyiso/Nyimbo za Tohara
  • Zinazohusiana na tohara.

Mfano

Ewe kilizi

Ulozowea kujificha

Nyuma ya mama kujikinga, dhidi ya milio

ya radi ilo juu mbinguni

Jua kesho ni siku ya siku

Siku ya kujua mbichi na mbivu

Kutofautisha jogoo na vipora,

            Ngariba taposhika, chake kijembe

Ndipo utakapojua bayani

Ukoo wetu si wa kunguru

Ikiwa hu tayari

Kisu kukidhihaki

Sithubutu kamwe, wanjani kuingia

sije kuniaibisha miye, amiyo na akraba nzima!

Sifa

  1. Huambatana na shughuli za jando (wavulana) na unyago (wasichana).
  2. Huimbwa faraghani katika mazingira ya tohara pekee.
  3. Huimbwa usiku wa kuamkia siku ya tohara.
  4. Zilitoa sifa kwa waliotahiriwa, wazazi na wasimamizi wao.
  5. Ziliimbwa kuwapa wavulana ujasiri wa kukabili kisu cha ngariba.
  6. Zilitoa mafunzo kuhusu majukumu mapya baada ya kutahiriwa.
  7. Hujumuisha watu maalum walioteuliwa kushiriki katika sherehe.
  8. Huhusisha watu wa jinsia na umri fulani.
  9. Maudhui yake hutegemea jinsia.
  • Majukumu
  1. Kuonyesha vijana wamevuka kutoka utotoni hadi utu uzima.
  2. Kuwaandaa vijana kwa uchungu watakaouhisi kupitia kijembe.
  3. Kuhimiza ujasiri na ukejeli uoga.
  4. Kusifu wahusika kwa ujasiri wa kukabili kisu na kuingia katika utu uzima.
  5. Kuburudisha waliohudhuria shughuli ya jando au unyago.
  6. Kuelekeza vijana kwenye matarajio mapya ya jamii.
  7. Kufunza majukumu katika utu uzima.
  8. Kukuza umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuwaleta wanajamii pamoja.
    1. Mbolezo/Mbolezi
  • Nyimbo za kuomboleza.

Mfano

Nalitazama jua likichwa,

Matumaini yangu yakizama pamoja

na miale miekundu

Nalidhani lilikuwa jinamizi tu

Kwamba ulikuwa kesha n’acha

Walikuwa wameisha n’ambia

Walimwengu

Ela nilikataa katakata walosema

Nikajitia kuamini waloamba yalikuwa

Uzushi

Hadi siku hii nilopokea waraka,

Waraka ambao ulikuwajeneza ka kuzikia

Pendo letu la miongo miwili.

Sifa

  1. Huimbwa wakati wa maafa, kifo, makumbusho ya mtu au kushindwa katika jambo k.v. vita.
  2. Huimbwa kwa sauti ya chini.
  3. Hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.
  4. Huwa na mapigo ya polepole au taratibu.
  5. Huimbwa kwa toni ya huzuni/uchungu kuibua hisia za ndani za mwombolezaji.
  6. Aghalabu haziandamani na ala.

Majukumu

  1. Kuwafariji au kuwasaidia waliofiwa kukabiliana na uchungu wa kupoteza mpendwa wao.
  2. Kusifu aliyekufa kwa kutoa sifa zake chanya au michango yao.
  3. Kubembeleza roho za wafu(mizimu) ili kusitokee maafa mengine.
  4. Kuonyesha msimamo wa jamii kuhusu matokeo ya kifo k.v. husababishwa na pepo, maovu, njia ya kuingia mbinguni.
  5. Kutakaswa hisia za huzuni za aliyefiwa kumpunguzia uzito wa kumpotezea mpendwa wake.
  6. Kueleza kutoepukika kwa kifo.
  7. Kukejeli kifo.
    1. Nyimbo za Taifa
  • Nyimbo zinazoimbwa na watu wa taifa fulani.

Majukumu

  1. Kutambulisha taifa fulani.
  2. Kuonyesha utaifa.
  3. Kuonyesha uzalendo (mapenzi kwa nchi).
  4. Kuhimiza uzalendo.
  5. Kukashifu wasio wazalendo.
  6. Kusifu taifa fulani.
  • Nyimbo za Siasa
  • Zinazoimbwa katika shughuli za kisiasa.

Mfano

Ewe mainga wa Ndumi

Siwe uloambia akina mama

Siku tulopiga foleni

Chakula cha msaada kupata

Turudishe vifaranga kwenye miji

Wageuke vijusi tena

Njaa isiwaangamize?

 

Siwe ulopita

Matusi ukitema

Chumvi na sukari kuturushia ja samadi?

Ukatununua vihela uloturushia

Ukatununua kura ukapata?

Sasa miaka mitano imetimia

Waja tulaghai tena

Huna lolote safari hii

Ubunge umekudondoka ukitazama

Wanyonge tumea/mua

Kwingine kujaribu

Majukumu

  1. Kuburudisha watu katika shughuli za kisiasa.
  2. Kupinga dhuluma za viongozi.
  3. Kusifu viongozi na sera zao.
  4. Kukashifu/kukejeli wanasiasa wabaya.
  5. Kuonyesha matarajio ya watawaliwa kwa viongozi.
  6. Kusambaza elimu ya kisiasa.
  7. Kuwatia wananchi kasumba.
  8. Kueneza propaganda za kisiasa.
  9. Kuzindua au kuhamasisha jamii kisiasa.
  10. Kuliwaza wahasiriwa wa migogoro ya kisiasa.
  11. Kutia watu ari ya kufanya jambo fulani k.v. kupigania haki zao.
  • Nyimbo za Vita
    • Zinazoimbwa na askari vitani au baada ya vita.

Majukumu

  1. Kuburudisha washiriki.
  2. Kufunza namna ya kukabiliana na adui.
  3. Kujasirisha washiriki.
  4. Kusifu askari vitani.
  5. Kukejeli uoga.
  6. Kusifu mashujaa wa zamani.
  7. Kukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga masujaa.
    • Kongozi
      • Za kuaga mwaka katika jamii za waswahili.
  1. Jadiiya
    • Nyimbo za jadi ambazo hupokezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
    • Huhusu matukio ya kihistoria k.v. shujaa, mateso, njaa, n.k.
  • Nyimbo za Kuzaliwa kwa Mtoto
  • Za kuonyesha au kuadhimisha kuzaliwa kwa mtoto.
    1. Maghani
  • Ushairi ambao hutolewa kwa kalima.

Sifa

  1. Husimulia matukio kwa kirefu hasa yanapotambwa.
  2. Hutolewa kwa kalima.
  3. Hutungwa papo hapo.
  4. Hutongolewa mbele ya hadhira
  5. Hutungwa kwa ufundi mkubwa.
  6. Hutolewa na mtu mmoja au kundi la watu.

Aina za Maghani

  1. Maghani ya kawaida
  • Ambayo hugusia maswala ya kawaida kama mapenzi, siasa, harusi, kazi, maombolezo n.k.
  • Husemwa/huganwa tu bila kusimuliwa.
  1. Maghani Simulizi
  • Maghani ambayo husimulia hadithi kuhusu tukio la kihistoria.
  • Huhusu, mtu, tukio, kitu, mnyama, n.k.

Sifa

  1. Hutokea kama hadithi.
  2. Husimulia tukio la kihistoria.
  3. Ni ndefu.
  4. Waimbaji wake huitwa manju/yeli.
  5. Huandamana na ala kama zeze, marimba, n.k.

Tofauti kati ya maghani ya kawaida na maghani simulizi

Maghani ya kawaida Maghani simulizi
ü  Ni fupi.

ü  Haitumii ala.

ü  Huhusu maswala ya kawaida.

ü  Husemwa.

ü  Ni ndefu .

ü  Hutumia ala.

ü  Kihistoria.

 

 

ü  Huimbwa.

Maghani ya Kawaida

  1. Vivugo/majigambo
  • Utungo wa kujisifu au kujigamba.

Sifa

  1. Hutungwa baada ya ushindi wa harakati ngumu k.v. kesi, kumuua simba, kuoa msichana aliyependwa na wengi n.k.
  2. Fanani ni mwanamme.
  3. Hutungwa papo hapo.
  4. Hutungwa na kughanwa na mhusika mwenyewe.
  5. Hutumia chuku k.m. kujisifu kupita kiasi.
  6. Anayejigamba hujipa jina la kiistiari k.m. mnyama.
  7. Mhusika huvaa maleba yanayooana na tukio analojisifia.
  8. Kuna kutaja jina na ukoo wa baba na mama.
  9. Anayejisifu huahidi kutenda maajabu zaidi.
    1. Pembezi/pembejezi
  • Aina ya tondozi inayokusudiwa kusifu watu aina fulani katika jamii kutokana na matendo au mchango wao.
  • v. watawala, walezi wazuri, mashujaa wa vita, waganga mashuhuri hata wapenzi waliopigania pendo lao.

Mfano

Nani kama wewe mama?

Nani anokufana ‘mwaitu’

Subira uliumbiwa

Bidii nd’o jina lako la pili

Moyo wenye heba

Msimamo usoyumba

Anoelekeza kwa imani

Anoadhibu kwa mapenzi makuu

Mzazi, mlezi na rafiki wa dhati

Tangu siku za kusimama dede.

  • Tondozi
  • Utungo wa kutukuza watu, wanyama na vitu.
  • v. watu mashuhuri, wapenzi, mifugo, miti mikubwa.

Mfano

Kipungu kipungu

Nani kama yeye?

Hashindiki kwa nia

Hashindiki kwa shabaha

Hulenga binguni

Hutia ghera kufikiwa peo

Peo zisofikika kwa wanokata tama

Kipungu, kipungu, hachi tufani za anga.

Maghani Simulizi

  1. Sifo
  • Tungo za kusifu watu kutokana na matendo yao ya kishujaa.
  • Sifa zake hukaribiana na za tenzi hasa ikiwa ni shujaa anasifiwa.
  1. Tendi/tenzi
  • Ushairi mrefu unaoelezea maisha ya mashujaa tangu kuzaliwa hadi kufa kwao.
  • v. Utenzi wa Fumo Liyongo, Sundiata, Shaka Zulu, Wang`ombe waihura n.k.

Mfano

Asiyemjua mjua aliongwe atamjua

Namjuza kwa sifa zake alizokuwa nazo

Alisimika ufalme uliosifiwa

Akawa shujaa asiyetishwa

  • Utungo huu waweza kuwa wimbo wa sifa au utendi!

Sifa

  1. Huwa masimulizi yanayotolewa kishairi.
  2. Hutoa wasifu wa shujaa.
  3. Huwa na matumizi ya chuku.
  4. Wahusika hupewa sifa zisizo kawaida (kiungu).
  5. Ni masimulizi mrefu.
  6. Matumizi ya sitiari k.v. kulinganisha wasifiwa na wanyama wakali.
  7. Huangazia matendo ya mashujaa.
  8. Husimulia matukio ya kihistoria.
  9. Huimbwa pamoja na ala ya kimziki.
  10. Hutungwa papo kwa papo na kuhifadhiwa katika ubongo.
  11. Hujumuisha mbolezi zinazoonyesha anguko la shujaa.

Lengo

  1. Kuburudisha wanajamii.
  2. Kusifu mashujaa wa jamii.
  3. Kukuza uzalendo kwa kuhimiza wengine kuwaiga mashujaa.
  4. Kukuza ubunifu kwa kutunga papo hapo.
  5. Kuimarisha uwezo wa kukumbuka kwa kutungwa na kuhifadhiwa akilini.
  6. Kuburudisha waliohudhuria sherehe ampapo yanatolewa.
  7. Kuhifadhi na kuendeleza tamaduni za jamii
  8. Kukuza ufasaha wa lugha kwa fanani.
  9. Kufunza maadili.
  • Rara
  • Hadithi fupi na nyepesi za kishairi zenye visa vya kusisimua.

Mfano

Alichukua mkoba wake

Akanipa kisogo

Kana kwamba hakunijua

Kana kwamba hakusema, “Hadi mauko”.

 

Hakujali penzi letu

Hakujali wana

Ambao ndiye alowapa uhai

Alijua nilimpenda

Ila hata hilo alijipa kujipurukusha

Akayoyomea

Akamezwa na ulimwengu.

Sifa

  1. Huhusu mambo ya kubuni au ya kweli k.v. sherehe ya uhuru, kesi ya mauaji, n.k.
  2. Huhusu maswala ibuka na ya kawaida.
  3. Hadithi huwasilishwa katika beti.
  4. Huandamana na ala za mziki.
  5. Hutolewa kwa toni ya kitanzia.
  6. Huwa na visa vya kusisimua.
  7. Huwa na ucheshi wenye kinaya.
  8. Maswala hayatoleai kwa uwazi bali hufumbwa na kudokezwa.
  9. Huwa na uigizaji/utendaji.
  10. Mambo yanayosimuliwa hupigwa chuku.
  • Rara nafsi
  • Ushairi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake mwenyewe.

Mfano

Muda umefika wa pingu kutiwa

Kutiwa silisili, kwani si utashi wangu

Ukoo waniuza, mithili ya kondoo sokoni

Mwambieni shangazi kwaheri nampigia

Hata angataka kuniopoa hawezi

Kwani mahari imetolewa

Mifugo kikwi nduguye amepokea

Kwaheri mama, kwaheri dada.

Sifa

  1. Hugusia maswala yanayoathiri hisia za mtu binafsi kama vile mapenzi, usaliti, talaka, kifo.
  2. Huwasilishwa kwa njia ya uimbaji unaoandamana na ala ya mziki.
  3. Mzungumzaji huzungumza moja kwa moja na hadhira au aliyeandikiwa rara hii-mkewe, mpenziwe, mwanawe, Mungu, miungu.
  4. Hutolewa katika miktadha k.v. mazishi kusifu aliyekufa, harusi na Bi. Arusi kama ameshinikizwa kuolewa.
    1. Ngonjera
  • Mashairi ya kujibizana/kulumbana-yenye muundo wa kimazungumzo.

Sifa

  1. Huwa na wahusika wawili au zaidi.
  2. Mhusika mmoja huuliza jambo na mwingine hujibu.
  3. Huendelezwa kwa njia ya wimbo.
  4. Wahusika kupingana mwanzoni.
  5. Wahusika huafikiana kufikiwa mwisho.

Umuhimu

  1. Majibizano hukuza ubunifu kwa kila mmoja kuonyesha umaarufu.
  2. Kukuza ujasiri wa kuzungumza hadharani.
  3. Kuimarisha stadi ya kuongea.
  4. Kuburudisha hadhira.
    1. Mashairi Mepesi.
  5. Mashairi ya kawaida ambayo hupatikana katika ushairi simulizi.
  6. Hujumuisha mashairi mafupi ya kihisia, kimapenzi, kusifu na kukosoa watu.

Vigezo vya Uchanganuzi wa Tungo za Ushairi Simulizi

  1. Kuainisha utungo kimaudhui/aina
  2. Kuthibitisha ni aina fulani ya utungo wa kishairi/sifa.
  3. Kutaja sifa zinazojitokeza za ushairi simulizi/utungo fulani wa ushairi simulizi.
  4. Muktadha ambamo unaweza kutolewa.
  5. Kuandika mbinu za kifasihi zilizotumiwa katika utungo huo.
  6. Kufafanua sifa za jamii zinazojitokeza katika utungo.
  7. Kuandika majukumu ya aina hiyo ya utungo wa ushairi katika
  8. Anayeimba/nafsi imbi ni nani?
  9. Kuandika maadili yanayojitokeza katika utungo.
  10. Kueleza toni ya utungo huo.

MAZUNGUMZO

  • Maongezi ya mdomo yenye usanii.

Sifa

  1. Huwa maongezi yenye usanii mkubwa.
  2. Hutolewa mbele ya hadhira.
  3. Hutolewa mbele ya hadhira.
  4. Hutolewa kwa njia isiyokera.
  5. Huambatana na sherehe fulani k.m. taabili katika matanga.
  6. Hutegemea sauti na vitendo.
  7. Huhusisha matumizi ya ishara k.v. za uso, mikono na miondoko.
  8. Huhitaji ustadi wa kuzungumza ili kuteka hadhira.
  9. Hutolewa na watu wenye umilisi mkubwa wa lugha.

Vipera vya Mazungumzo

  1. Hotuba
    • Maelezo yanayotolewa mbele ya watu kuhusu mada fulani.
    • Huhusisha mada maalum sio suala lolote tu.

Umuhimu

  1. Kuelimisha kwa kupa maarifa ya kukabiliana na maisha k.v. jandoni na arusini.
  2. Kuadilisha au kutoa nasaha hadharani.
  3. Huimarisha ukakamavu wa kuzungumza kadiri watu wanavyotoa hotuba hadharani.
  4. Kukuza ufasaha na umilisi wa lugha.
  5. Kupalilia kipawa cha uongozi.
  6. Kuelimisha kwa kupatia watu maarifa ya kukabiliana na changamoto za maisha.

Aina za Hotuba

  1. Risala
  • Hotuba inayowasilishwa mbele ya watu kueleza jambo fulani k.m. ya wafanyakazi kwa waajiri wao.
  1. Mhadhara
  • Hotuba inayotolewa kwa hadhira fulani kufafanua somo au mada fulani.
  1. Kumbukizi
  • Hotuba zinazohusu tukio fulani la kihistoria kuhusu mtu au kitu.
  1. Mahubiri
  • Hotuba zinazohusu masuala ya kidini.
  1. Taabili
  • Hotuba kuhusu aliyeaga dunia zinazohusu sifa zake nzuri.
  1. Malumbano Ya Utani
  • Mazungumzo ya kutaniana.

Aina

  1. Utani wa mawifi na mashemeji
  2. Utani wa marafiki
  • Utani wa vijana
  1. Utani wa watoto
  2. Utani wa marika/ watu wa hirimu moja
  • Wewe ni mweusi kiasi kwamba ukiingia chumbani taa zinazimika.
  1. Utani wa mababu/mabibi na wajukuu
  • Ee mume wangu, mbona walala mapema hivi? Utawezaje kulilinda boma letu ikiwa wewe ndiwe wa kwanza kujizika kitandani.
  • Utani wa maumbu (ndugu na dada)
  • Wewe unajifanya jasiri na juzi baba alikukemea kidogo tu ukaanza kutetemeka kama kondoo aliyenyeshewa.
  • Utani wa mazishi
  • Afadhali umekufa tukakuzika, sasa maghala yetu yatasalimika.
  1. Utani wa makabila/ki ukoo
    • Wakikuyu wanapenda pesa kiasi kwamba maiti ikisikia mlio wa sarafu inaweza kufufuka.
    • Wakamba wa ukoo wa Akanga wanapenda nyama kiasi cha kula kijusi cha mbuzi.

Sifa

  1. Huwa kati ya watu wawili au makundi mawili ya watu.
  2. Hufanywa kwa kujibizana papo hapo.
  3. Hufanywa kwa njia isiyo ya kuudhi.
  4. Hutumia maneno ya mizaha.
  5. Hutumia lugha ya ucheshi.
  6. Hufanywa na watu wenye uhusiano mzuri.
  7. Huchukua njia ya ushindani kila mmoja akitaka kumpiku mwenzake.
  8. Watanianao huwa wamekubaliana kufanya hivyo.
  9. Hufanyika katika wakati unaofaa sio baada ya kukutana tu.
  10. Huhusisha masimango au kumkumbusha mtu wema uliomtendea.
  11. Hutumia chuku sana kusisitiza au kukejeli sifa fulani hasi.
  12. Huhusisha wakati mwingine utaniaji wa wasiokuwepo ukiambatanishwa na uigizaji wa kuchekesha.
  13. Hutegemea uhusiano ulio kati ya wanajamii au makabila.
  14. Huandamana na sherehe kama matanga.

Umuhimu

  1. Kuburudisha kutokana na ucheshi.
  2. Kuimarisha urafiki wa watu walio na uhusiano mwema wanaotaniana.
  3. Hustawisha ufundi wa lugha.
  4. Kukashifu tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, wivu, n.k.
  5. Kukosoa wanajamii kwa njia ya kejeli/dhihaka
  6. Kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya wahusika.
  7. Kuliwaza k.m. unaofanywa wakati wa maombolezo.
  8. Kukuza na kudumisha mila na desturi za jamii.
  9. Kukuza utangamano baina ya watu na wanajamii wanapokuja pamoja na kutaniana.
  10. Kuhimiza watu kujieleza kwa uwazi kwa kupunguza urasmi miongoni mwa wanajaii.
  11. Hudhihirisha uhusiano mwema baina ya watu wa jamii fulani.

Changamoto Sasa

  1. Mabadiliko katika jamii yaliyosababisha baadhi ya wanajamii kupoteza nyenzo hii.
  2. Kuingiliana kwa watu wa jamii mbalimbali.
  • Soga
  • Mazungumzo ya kupitisha wakati yasiyozingatia mada maalum.

Sifa

  1. Hutokea baina ya watu wa rika moja.
  2. Humithilisha uhalisia badala ya kuunakili.
  3. Hutumia chuku na kufanywa ljambo lionekane kama halina uhalisia.
  4. Hukejeli watu au hali fulani.
  5. Wahusika ni wa kubuni.
  6. Hutumia vichekesho kupunguza ukali wa ukweli uliomo.
  7. Wahusika hupewa majina ya wanajamii husika.
  8. Huwa na mafunzo au maadili.

Umuhimu

  1. Kuburudisha kwa kuchekesha.
  2. Kufunza maadili.
  3. Kukejeli matendo yasiyofaa katika jamii
  4. Kukuza ubunifu baina ya washiriki.
  5. Kufunza kuhusu matendo na tabia za kibinadamu.
  6. Huwa msingi wa utani unaokuwapo katika jamii.
  7. Kuonya na kutahadharisha dhidi ya tabia siyokubalika.
  • Mawaidha
  • Mazungumzo ya kutoa ushauri kuhusu jambo fulani.

Sifa

  1. Huwasilishwa mbele ya watu.
  2. Hugusia takriban vipengele vyote vya maisha ya binadamu.
  3. Aghalabu hutolewa na watu wenye umri mkubwa.
  4. Hulenga maudhui maalum na ya aina nyingi kutegemea jinsia, umri, shughuli, n.k.
  5. Hutumia lugha ya kubembeleza na isiyoonyesha ukali.
  6. Hutumia lugha ya kuathiri hisia.
  7. Huwa na ufasaha mkubwa wa lugha.
  8. Ni mawazo mazito kuhusu maisha.
  9. Hutolewa katika miktadha rasmi na isiyo rasmi.
  10. Ujumbe hulenga hadhira maalum k.m. ya kike au kiume.
  11. Hutumia fani nyingine za fasihi kama methali, misemo, ngano, nyimbo n.k. kupitisha mawaidha.
  12. Huibua maadili yanayohitaji kuzingatiwa.

Muundo wa Mawaidha

  1. Utangulizi
    • Kutoa kauli ya kuvutia makini ya hadhira k.v. ‘Utu uzima huenda na uwajibikaji’, au kueleza kiini cha mawaidha.
  2. Mwili
  • Kutoa wosia, maonyo, maelekezo kutegemea suala analotolea mawaidha akitumia jazanda, kupanda na kushuka kwa sauti, kimya, miondoko, kubadilisha kasi ya kuzungumza, kudondoa semi za watu maarufu, n.k.
  1. Hitimisho
  • Kuonyesha msimamo kuhusiana na suala analozungumzia.
  • Kushirikisha hadhira ili kujua msimamo wao kuhusu suala alilowausia.
  • Hadhira kutoa changamoto kuhusiana na mawaidha yanayotolewa.

Umuhimu wa mawaidha

  1. Kuelekeza jamii kimaadili.
  2. Kuelekeza kuhusu jinsi ya kukabiliana na changa moto maishani.
  3. Kushauri jinsi ya kutenda jambo fulani.
  4. Kujasirisha waoga na kuwapa ukakamavu.
  5. Kuwaondolea wanajamii ujinga.
  6. Kuhifadhi na kuendeleza mila na desturi za jamii.
  7. Njia ya kipato kwa baadhi ya watu.
  8. Kuelimisha kuhusu maarifa ya kuendeshea maisha, majukumu na matarajio ya jamii.
  9. Ulumbi
    • Uwezo na ustadi wa kuzungumza kwa uhodari mkubwa.

Miktadha Ambamo Ulumbi Hutumika Katika Jamii

  1. katika mijadala mbungeni
  2. katika hotuba za kisiasa
  3. katika mahubiri maabadini
  4. katika mijadala shuleni
  5. kortini
  6. katika shughuli za kijamii k.v. posa
  7. katika sala/dua
  8. katika maapizo
  9. katika malumbano ya utani
  10. katika majigambo/vivugo

Sifa

  1. Hufanywa mbele ya hadhira.
  2. Huwa na lengo maalum k.v. kushawishi, kuelimisha, kushauri n.k.
  3. Hutumia tamathali za usemi kwa ufanifu mkubwa k.v. chuku, misemo, methali, n.k.
  4. Lugha huwa yenye mvuto na ufasaha.
  5. Hutumia lugha yenye taharuki na ushawishi.
  6. Unenaji huambatana na utumizi wa ishara/ viziada lugha.
  7. Uwasilishaji huwa sahili na wenye ujumbe mzito.
  8. Huwa na urudiaji mwingi ili kusisitiza na kuvutia usikivu.
  9. Huwa na matumizi ya taharuki k.v. mtuo.
  10. Huwa na mtiririko mzuri wa mawazo.

Sifa za Mlumbi

  1. Asiwe mwoga ili kuweza kuzungumza hadharani.
  2. Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidi.
  3. Awe mchanganfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai.
  4. Awe na ufahamu mpana wa utamaduni wa hadhira asitumie maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhira.
  5. Awe na uwezo wa kuingiliana vizuri na hadhira ili aivutie.
  6. Awe na kumbukumbu nzuri ili ulumbi wake utiririke vizuri.
  7. Awe na uwezo wa kudramatisha ili kuonyesha picha fulani k.v. ishara za uso, mwili, miondoko kuonyesha picha ya analozungumzia.
  8. Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
  9. Aweze kubadilisha toni na kiimbo hadhira isikinai.
  10. Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kwa maswali ya balagha ili kuondoa uchovu wa kusikiliza.
  11. Awe na uwezo wa kutumia mtuo wa kidrama ili kuongeza taharuki, kusisitiza ujumbe na kuteka makini ya hadhira.

Umuhimu

  1. Hukuza uwezo wa kujieleza na kusema hadharani kwa kujiboresha kadiri anavyoendelea.
  2. Kigezo cha kuteulia viongozi wa baadaye kwani ushawishi humtambulisha mlumbi kama mwenye uwezo wa kuongoza.
  3. Kuelimisha jamii kwa njia isiyochosha.
  4. Kudumisha umoja na ushirikiano jamii inapokusanyika pamoja kusikilizaulumbi.
  5. Kuhamasisha na kuzindua jamii juu ya suala fulani.
  6. Kushawishi walengwa wakubali jambo fulani.
  7. Kukuza uwezo wa mwanajamii kushawishi na kupatanisha.
  8. Kushawishi watu wapende jambo fulani.
  9. Kuburudisha wasililizaji.
  • Maapizo
  • Maombi maalum ya kumtaka Mungu, miungu au mizimu kumwadhibu mhusika hasidi, mkinzani au muovu.

Mfano

Ikiwa kweli wewe ni mkazamwanangu,

Nami ndiye nilompa uhai mwana unoringia,

Anokufanya upite ukinitemea mate,

Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,

Miungu nawaone chozi langu, wasikie kilio changu,

Mizimu nawaone uchungu wangu,

Radhi zao wasiwahi kukupa,

Laana wakumiminie,

Uje kulizwa mara mia na wanao,

Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,

Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha,

Wakazawanao wasikuuguze katika utu uzima wako!

Sifa

  1. Yalitolewa kwa waliokwenda kinyume na matarajio ya jamii.
  2. Yalifanywa mahali maalum k.v. makaburini, porini, chini ya miti mikubwa, n.k.
  3. Hutolewa kwa ulaji kiapo.
  4. Yalitolewa na mwathiriwa au watu maalum walioteuliwa.
  5. Maapizo huaminiwa yataleta maafa kwa jamii.
  6. Watoaji maapizo walikuwa walumbi.
  7. Maapizo hutumia lugha kali inayonuiwa kutia woga ili kutahadharisha dhidi ya maovu.

Umuhimu

  1. Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya maovu.
  2. Kutambulisha jamii kwani kila mojawapo ina aina yake ya kuapiza.
  3. Kukuza umoja katika jamii kwani kaida na miiko hufanya wanajamii kujihisi kuwa kitu kimoja.
  4. Kuadilisha wanajamii kwa kujifunza kutenda mema ili kuepuka laana.

MAIGIZO

  • Utanzu wa fasihi simulizi unaoambatana na vitendo.
  • Sanaa ya mazungumzo yanayoambatana na vitendo.

Sifa

  1. Huwa na watendaji au waigizaji.
  2. Huwasilishwa mbele ya hadhira.
  3. Huwasilishwa mahali maalum k.v. ukumbini.
  4. Huwasilishwa kwa mazungumzo na matendo
  5. Waigizaji hujivika maleba yanayooana kutia uhai maigizo.
  6. Matayarisho kabambe hufanywa kabla ya maigizo.
  7. Huweza kuambatana na ngoma pamoja na uimbaji.
  8. Lugha ni yenye ufundi wa juu k.v. picha, mafumbo na tamathali.
  9. Huweza kuambatana na sherehe fulani ya kitamaduni k.v. jando, matanga, n.k.
  10. Huwasilishwa kwa lugha sahili.
  11. Hujaa taswira zinazoweza kutambulika na hadhira.

Umuhimu

  1. Kuburudisha wahusika na hadhira.
  2. Kukuza umoja na ushirikiano kwa kujumuisha watu pamoja.
  3. Kuimarisha uwezo wa kuzungumza hadharani-kupata ukakamavu jinsi mtu anapoendelea kuigiza.
  4. Kukuza umoja na ushirikiano watu wanapojumuika pamoja kutazama maigizo.
  5. Kukuza uwezo wa kukumbuka kwani mwigizaji huhitaji kukumbuka maneno halisi.
  6. Kukejeli kitendo kisichofaa/cha kijinga alichofanya mtu.
  7. Njia ya kipato/kuwatafutia riziki baadhi ya watu.
  8. Kutoa nafasi kwa watu kudhihirisha vipawa vyao.
  9. Kuonya na kutahadharisha watu dhidi ya kufaya mambo yasiyofaa.
  10. Kuelimisha watu wafahamu jambo fulani k.v. ukimwi, ufisadi, n.k.
  11. Kukosoa watu wanaofanya kinyume na matarajio ya jamii k.v. wivu, uchoyo, n.k.
  12. Kupitisha maarifa na amali za kijamii.

Ploti

  1. Utangulizi-kutambulisha mgogoro
  2. Ukuzaji wa mgogoro
  3. Kilele cha mgogoro
  4. Usuluhishaji wa mgogoro

Aina za maigizo

  1. Maigizo Ya Kawaida
  • Maonyesho ya jadi yakiwa yameondolewa kwenye mazingira yake halisi.
    1. Sanaa ya Maonyesho
  • Matendo ya kweli yanayojitokeza katika jamii kulingana na mazingira yake halisi k.m. uganga, mazishi, unyago, ngoma, n.k.

Tofauti

Maigizo ya kawaida Sanaa ya maonyesho
ü  Mazingira ya kuzua/maalum

ü  Matukio ya kuiga

ü  Huwa na wahusika na hadhira maalum

ü  Matumizi ya ukumbi na jukwaa maalum

ü  Hutumia maleba na vifaa vya kuzua mazingira maalum

ü  Hugawika katika maonyesho Kutumia lugha kwa njia maalum

ü  Wahusika hufanya mazoezi kabla ya igizo halisi

ü  Hutumia mazingira halisi

ü  Matukio halisi/ ya kila siku.

ü  Washiriki na waigizaji walio pia hadhira

ü  akuna haja ya ukumbi wala jukwaa

ü  Hakuna vifaa maalum bali huwa mazingira yenyewe.

 

ü  Muundo wake hufululuza au hayajagawika katika maonyesho.

 

ü  Hawahitaji kufanya mazoezi kwani ni matukio ya kila siku.

 

Maigizo ya kawaida

  1. Michezo ya Kuigiza
  • Maigizo ambayo huwasilishwa na watendaji jukwaani mbele ya watu.

Sifa za Mwigizaji bora

  1. Awe jasiri ili aweze kuigiza mbele ya watu/hadharani.
  2. Awe na ubunifu ili aweze kufanya uigizaji kuvutia na kuondoa ukinaifu.
  3. Awe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kuonyesha picha ya hali anayoigiza.
  4. Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
  5. Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza k.v. huzuni.
  6. Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa maswali ya balagha ili kuondoa uchovu.
  7. Awe na uwezo wa ufaraguzi/ kubadilisha uigizaji wake papo hapo kutegemea hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira.
  8. Awe anaelewa utamaduni wa hadhira yake ili asitumie maneno na ishara ambazo zinaudhi ama kukinzana na na imani zao.
  1. Vichekesho
    • Michezo ya kuigiza inayokusudiwa kuzua kicheko ili kupitisha ujumbe k.m. vioja, vitimbi n.k.

Sifa

  1. Vichekesho huigizwa.
  2. Huwasilishwa kwa lugha sahili.
  3. Hujaa taswira zinazoweza kutambulika na hadhira.
  4. Hutumia mbinu ya kejeli, kunaya na tashtiti.
  5. Vichekesho huwa vifupi.
  6. Havihitaji uchambuzi wa ndani ili kuvielewa au kupata maana.

Jukumu

  1. Kuburudisha hadhira kwa kuchekesha.
  2. Kuelimisha kwa kuonyesha jambo la kijinga alilofanya mtu.
  3. Njia ya kuwapatia watu riziki.
  4. Hutumika katika hadithi kuifanya ivutie.
  5. Kukejeli kitendo fulani kisichofaa alichofanya mtu fulani.
  6. Kukashifu matendo hasi ya kijinga.
  7. Kuadilisha ama kutoa funzo fulani la tabia njema.
    • Ngonjera
    • Ngonjera inayoambatana na uigizaji/utendaji.

Sifa

  1. Kuweko kwa uigizaji/utendaji k.v. ishara za uso na mikono.
  2. Huwa na wahusika wawili au zaidi.
  3. Huendelezwa kwa njia ya wimbo.
  4. Mhusika mmoja huuliza jambo na mwingine hujibu.
  5. Wahusika kupingana mwanzoni.
  6. Wahusika hufikia uafikiano kufikia mwisho.
  • Michezo ya Watoto/Chekechea
  • Michezo inayoigizwa na watoto katika shughuli zao.

Aina

  1. Mchezo wa baba na mama
  2. Kuruka kamba
  3. Kujificha na kutafutana
  4. Kukimbiza kibaramwezi dhidi ya upepo ili kizunguke
  5. Mchezo wa baba na mama

Sifa

  1. Waigizaji ni watoto.
  2. Huhusu shughuli za kiuchumi na kitamaduni k.v. arusi, siasa, ukulima.
  3. Huandamana na nyimbo za watoto.
  4. Huwa na miondoko mingi k.v. kujificha, kuruka.
  5. Huwa na matumizi mengi ya takriri.
  6. Huchezwa popote.
  7. Huwa na kanuni fulani.
  8. Hukoma watoto wakichoka au wakikiuka kanuni

Umuhimu

  1. Kufunza watoto majukumu yao ya utu uzima.
  2. Kuwatanguliza watoto katika sanaa ya uigizaji.
  3. Kukuza ubunifu wa watoto kadiri wanapoendelea kuigiza.
  4. Kudumisha utamaduni wa jamii.
  5. Kuburudisha watoto.
  6. Kukuza stadi ya uigizaji miongoni mwa watoto.
  7. Kukuza utangamano miongoni mwa watoto kwa kuwajumuisha pamoja.
  8. Kukashifu matendo hasi ya watu wazima kwa watoto.
  9. Kuwapa watoto ukakamavu na kujiamini wakiwa wachanga.
    1. Majigambo/vivugo
  • Uigizaji ambapo wahusika hujigamba kwa matendo ya kishujaa.

Mfano

Ndimi Kisoi, dume la ukoo mtukufu

Ulojipamba kwa mabingwa

Wachezaji hodari wa ngoma

Ndimi dume liloingia nyanjani

Makoo yakatetemeka

Yakang’ang’ania, ngozi kusakata nani

 

Kijiji kizima kilinijua

Wazee walilienzi

Wakamiminika kiamboni

Mabinti kunikabithi.

Sifa

  1. Aghalabu huambatana na ngoma.
  2. Hujitokeza, kujigamba na kisha kuendelea kucheza ngoma.
  3. Anayejigamba hubeba zana zake za vita kama vile mkuki na ngao kuonyesha aliyotenda.
  4. Anayejigamba huvaa maleba kuambatana na jambo analojisifia.
    • Utambaji
    • Usimulizi wa hadithi unaoambatana na uigizaji.
    • Huwa na matumizi ya vizuizui.
    • Mazingira
  • Uigizaji wa maumbile asilia yaliyozunguka jamii ya watu k.v. sauti za wanyama.
  • Kuna matumizi ya viziuzui, matawi n.k.

Sanaa ya Maonyesho

  1. Ngoma
  • Uchezeshaji wa viungo vya mwili kuambatana na mdundo au miondoko maalum.

Aina

 

  1. Ngoma za wanawake
  2. Ngoma za tohara
  3. Ngoma za wanaume
  4. Ngoma za sherehe
  5. Ngoma za vijana
  6. Ngoma za unyago na jando
  7. Ngoma za wazee
  8. Ngoma za arusi
  9. Ngoma za kufukuza mapepo
  10. Ngoma za kuaga mwaka

 

 

Sifa

  1. Huandamana na muziki na ala ya muziki k.v. ngoma.
  2. Ngoma huchezewa mahali wazi na penye hadhira.
  3. Wachezaji huvaa maleba maalum kulingana na funzo linalonuiwa.
  4. Huwa na wahusika aina mbili; watendaji na watazamaji kwa wakati mmoja.
  5. Huweza kuandamana au kutoandamana na sherehe.
  6. Hutofautiana kulingana na jamii husika.

Umuhimu

  • Kuburudisha kwa ufundi wa kucheza kwa kuzingatia miondoko.
  • Kitambulisho cha jamii kwani kila moja ina aina yake ya ngoma.
  • Kuhifadhi na kuendeleza tamaduni za jamii husika.
  • Kukuza uzalendo kwa kuwafanya wanajamii kuionea fahari jamii yao.
  • Kukuza umoja na ushirikiano kwa kujumuisha watu pamoja.
  • Kuelimisha kwa kupitisha mafunzo na maarifa.
    1. Matambiko
  • Utoaji wa kafara kwa Mungu, miungu, pepo au mizimu ili wasaidiwe kutatua shida, kutoa shukrani au kuomba radhi.

Sifa

  1. Hutolewa na wazee maarufu walioteuliwa.
  2. Hufanywa nahali maalum k.v. pangoni, mwituni, n.k.
  3. Huandamana na sala.
  4. Huandamana na utoaji kafara k.v. kuchinja mbuzi, n.k.
  5. Huandamana na maombi.
  • Maigizo Ya Uganga wa Ramli

Sifa

  1. Mganga hujitia kujua kwa hivyo vitendo vyake ni maigizo ya uganga wa madaktari.
  2. Mengi katika matendo ya mganga hayana mashiko.
  3. Aghalabu kafara hutolewa.
  4. Waganga wanapopiga bao huvaa maleba kama ngozi, vibuyu, pembe, n.k.
  5. Huweza kuwa na fimbo maalum.
  6. Lugha maalum anayodai kuitumia kuwasiliana na misimu.
  7. Mizimu humshauri mganga kuhusu ugonjwa na tiba inayofaa.
  8. Mganga humchanja mgonjwa na kumpa dawa za miti shamba.

Umuhimu

  1. Wakati mwingine mizizi ya mganga huponya.
  2. Huwapa watu matumaini hasa walio na magonjwa yasiyo na tiba.
  3. Dawa za mganga hupunga mashetani kwa wagonjwa wake.
  4. Hukutanisha ulimwengu wa mizimu na ulimwengu halisi.
  5. Waganga huburudisha wanapoigiza.

Hasara

  1. Mgonjwa huenda asipone kwani matendo mengi ya mganga ni ya kukisia.
  2. Dawa za uganga zaweza kumdhuru mtu.
  3. Malipo ni ghali na mtu hata aweza kufilisika akitafuta tiba ya ugonjwa usiopona.
  4. Mazingira ya uganga husheheni uchafu mwingi.
  5. Mgonjwa huridhika kwa muda mfupi halafu uhalisia hudhihirika.
    1. Ngomezi
  • Uwasilishaji wa ujumbe kwa kupiga ngoma au zana nyingine ya kimziki.

Sifa

  1. Kuwepo kwa ngoma au ala nyingine kama panda.
  2. Mapigo ya ngoma hueleweka tu na jamii husika.
  3. Mapigo kufuata toni au ridhimu maalum kuwasilisha maneno fulani.
  4. Kuwepo kwa hadhira au wasikilizaji.
  5. Kueleweka kwa mapigo hayo na wanajamii husika pekee.
  6. Makini huhitajika ili kupata midundo.

Aina za ngomezi

  1. a) Taarifa
  • Huarifu kuhusu jambo k.m. msimu wa kuanza kutayarisha mashamba, kuitwa katika mkutano, kazi ya ujima n.k.
  1. b) Tahadhari
  • Hutoa tahadhari kuhusu mavamizi kama wizi wa mifugo, vita, majanga kama moto, mafuriko n.k.
  1. c) Uhusiano
  • Kuita watu kwa sherehe.

Umuhimu wa Ngomezi

  1. Njia ya mawasiliano kwa jamii zisizojua kusoma.
  2. Husaidia wanaokabiliwa na ugumu wa mawasiliano.
  3. Kuharakisha mawasiliano katika masafa mafupi.
  4. Kutoa taarifa kuhusu matukio fulani k.m. ndoa, kifo n.k.
  5. Husaidia kupitisha jumbe za dharura.
  6. Kutahadharisha wanajamii kuhusu tukio la hatari/dharura k.v. vita, gharika n.k.
  7. Kuficha siri kwa kuwasilisha ujumbe kwa njia isiyoeleweka.
  8. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii.
  9. Namna ya kudhihirisha ufundi wa kutumia zana kama ngoma.
  10. Kitambulisho cha jamii kwani kila jamii hupitisha ujumbe kwa mapigo tofauti.

Udhaifu wa Ngomezi

  1. Si kila mtu anaweza kufasiri ujumbe unaokusudiwa.
  2. Mapigo hayasikiki mbali na hivyo husikika na idadi dogo ya watu.
  3. Mapigo yaweza kuhitilafiana na hivyo kufasiriwa kwa namna tofauti.

Ngomezi za kisasa

  1. Milio ya ambulensi, magari ya polisi na zimamoto.
  2. Kengele za kubisha hodi nyumbani zinazotumia umeme.
  3. Kengele shuleni, makanisani, n.k.
  4. Toni za rununu zinazowakilisha aina mbalimbali za jumbe.
  5. Ving’ora vya kuashiria moto umetokea katika majumba ya horofa, benki, hospitalini, n.k.

Changamoto za Ngomezi katika Jamii ya Sasa

  1. Mwingiliano wa jamii mbalimbali unaosababisha kutofasiri ujumbe kwa njia moja inayotakikana.
  2. Viwanda na majumba marefu kusababisha kutosikika kwa sauti au milio ya ngoma.
  3. Njia nyingine za kisasa za mawasiliano zinazotumiwa kwa wingi na kwa wepesi.
  4. Uhaba wa zana kama baragumu na zumari zilizokuwa zinatumika.
  5. Mabadiliko ya maisha kuleta ubinafsi na kusababisha wengi kutoitikia wito wa vyombo.
    1. Mivigha
  • Sherehe za kitamaduni ambazo hutokea katika kipindi fulani cha mwaka ambazo huonyesha mwanajamii ametoka kiwango kimoja hadi kingine.

Aina za Mivigha

  1. Sherehe za tohara
    • kutoka utotoni na kuingia utu uzimani.
  2. Sherehe za ndoa
  • kutoka kapera hadi kuoa
    1. Sherehe za kutambika
  • kutoa sadaka kwa Mungu, miungu, pepo au mizimu
    1. Sherehe kutawazwa kwa kiongozi
  • kutoka uraia na kuingia katika uongozi/utawala
    1. Shughuli za mazishi/matanga
  • kutoka uhai hadi ufu
    1. Sherehe za kuwapa watoto majina
    2. Sherehe za ulaji kiapo
    3. Shughuli za posa
    4. ibada

Hatua

  1. Kutoa mtu rasmi kutoka kundi moja la wanajamii.
  2. Kumfundisha majukumu yanayohusiana na wadhifa mpya.
  3. Kumwingiza rasmi katika kundi jingine.

Sifa

  1. Huandamana na matendo au kanuni fulani (mivigha).
  2. Maleba maalum huvaliwa na wahusika kuwatofautisha na hadhira.
  3. Hufanyika kwa kutumia lugha maalum au kimyakimya.
  4. Kuna watu aina tatu: watendaji wanaoshiriki kuimba na kucheza, wale sherehe inafanyika kwa sababu yao na wanaoshuhudia tu.
  5. Huhusisha vitendo maalum kama kula viapo, kutoa kafara, kucheza ngoma, n.k.
  6. Huandamana na utoaji wa mawaidha.
  7. Uigizaji hujitokeza pale mwanajamii anaingizwa katika kundi fulani kutoka jingine.
  8. Huhusisha maombi.
  9. Hufanywa mahali maalum sherehe hiyo inapofanyika k.m. tambiko hufanywa porini au pangoni.
  10. Wahusika huweka ahadi za kutenda wema.
  11. Huwa na mpangilio wa shughuli kuanzia mwanzo, kati hadi mwisho.

Umuhimu

  1. Kuburudisha kwa vile baadhi ya mivigha huhusisha nyimbo, ngoma na uigizaji.
  2. Kutoa mafunzo ya utu uzima na elimu ya jadi.
  3. Mivigha ya mazishi huliwaza wafiwa.
  4. Kukuza utangamano miongoni mwa wanajamii kwa kuwajumuisha pamoja katika mivigha yao.
  5. Kuashiria mwanajamii ametoka kiwango kimoja cha maisha hadi kingine.
  6. Kujenga uhusiano bora kati ya jamii na miungu au mizimu.
  7. Kitambulisho cha jamii kwani kila moja ina aina yake ya mivigha.
  8. Kudumisha mila za jamii.
  9. Kuelimisha jinsi ya kukabiliana na changamoto maishani.
  10. Kuadilisha kwa kufunza tabia zinazokubalika na jamii k.v. uaminifu, utiifu, n.k.
  11. Kukashifu vitendo vya uoga.
  12. Kukuza uzalendo kwa kuhimiza wanajamii kuonea fahari tamaduni zao.
  13. Msingi wa wanajamii kujitambulisha na kuionea fahari jamii yao.

Hasara

  1. Baadhi ya mivigha huhatarisha afya na maisha k.v. kutahiri watoto wa kike.
  2. Baadhi ya sherehe hukiuka maadili kama vile kwa kuruhusu matusi hata kushiriki ngono.
  3. Baadhi yaweza kusababisha hasara kama vile kueneza ukimwi k.v. tohara kwa kisu kimoja.
  4. Huzua tofauti za kijinsia k.v. mwanamme kujiona bora kuliko mwanamke.
  5. Kuzua utabaka baina ya waliopashwa na wasiopashwa tohara.
  6. Baadhi ya mivigha hukiuka malengo ya kitaifa k.m. ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu
  7. Kunayo hujaza watu hofu k.v. kufukuza mapepo kunakohitaji kafara ya binadamu.
  8. Baadhi huhusisha ushirikina na hivyo kusababisha uhasama baina ya koo.
  9. Baadhi hugharimu kiasi kikubwa cha pesa na kuifilisi familia.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top